DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hautakuwa wa kawaida bali utakuwa uwanja wa mapambano ya kuikomboa demokrasia ya Tanzania, ambayo kimeeleza kuwa imetekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Shangwe Ayo, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Town School, kata ya Kambarage, Wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya Oparesheni Majimaji – kampeni ya kitaifa ya chama hicho ya kuhamasisha wananchi kulinda kura zao.
Shangwe amedai kuwa ushindi wa mara kwa mara wa CCM unatokana na matumizi ya hofu na mbinu zisizo za haki, akiwataka wananchi wa Shinyanga na Watanzania kwa ujumla kuwa na ujasiri wa kusimama dhidi ya vitisho hivyo.
Pia amegusia mwenendo wa chaguzi ndogo na mchakato wa uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wapiga kura kwa wingi na kuwalinda wagombea wanaotokana na wananchi wenyewe.
Ziara hiyo ya Oparesheni Majimaji imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kuimarisha mtandao wa ulinzi wa kura, uhamasishaji wa kisiasa, na kuwapa wananchi mbinu za kikatiba na kisheria za kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.