Shangingi La Serikali "Overtime"

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
M

MegaPyne

Guest


Yaelekea ni katika ile mbuzi ula kwa urefu wa kamba yake au pengine ni katika kujiongezea kipato cha ziada pale dereva wa Shangingi hili mali ya serikali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kule EPZA Bw Geofrey Ernest Barweta alipoamua kupiga ka-overtime kidogo kwa kutumia mshangingi huo pamoja na wenzie watatu kwenda kupora fweza katika kituo kimoja cha mafuta na kwa bahati mbaya kwao siku hiyo (sidhani kama hii ni mara ya kwanza) gemu likabumbuluka na kutiwa mbaloni (From Bongo Pix)

The Picture says it all.
 
Hii ni jokes au kweli?

Huenda ni kweli, lakini pia tujiulize hali halisi, dereva analipwa mshahara 100,000 kwa mwezi, na kakabidhiwa gari la milioni 200.

Niliwahi shuhudia mwingine akipiga debe 'live', magome 100, mwenge 200, akasanya abiria wake ambapo nami nilikuwa mmojawapo wa abiria. Mle ndani akawa sincere kabisa kwamba jamani sasa mi nifanyeje, gari kuuubwa, lakini hata 100 mfukoni sina.

Well, sishabikii kwamba wafanye uharifu, lakini malipo ya watu kama hawa wanaopewa dhamana ya vitu vya mamilioni inabdi yasiwe ya kusuasua namna hii ili pia kusaidia kuwaepusha na vishawishi kama hivi.
 

Tatizo utamlipa kiasi gani asiwe na tamaa? hahaha. Maana gari ndiyo hivyo la bei ghali na hata umlipe vipi bado kiwango cha mshahara hakiwezi kuwiana na gari lenyewe. Kama wabunge wenyewe hulipwa milioni 12 kwa mwezi na bado wanataka kuongezewa unategemea kuna anaye ridhika mkuu?
 

Nijuavyo mimi wabunge bwanalipwa karibu million 7 na kwa sasa mipango ipo ya kudai walipe 12! Chakushangaza 150,000/= inakatwa kodi lakini million 7 hazikatwi koko huu ni ukora mkubwa.
Viongozi wangekuwa mfano wa kulipa kodi hata walalahoi wasingelalamika sana!
 
Kuna dereva mmoja wa iliyokuwa RTD,alikuwa ktk kipindi cha twende na wakati yeye aliuza gari la RTD akiwa amelipaki pale CCM TANDALE na kusingizia limeibiwa.Walinzi wa CCM wako jela hadi leo wakati yule dereva amestaafishwa na kulipwa marupurupu yake na sasa anaishi maisha yanayomfaa Mbagala.Jamani hawa madereva wakuwaangalia sana wanaweza kukuuza hata wewe mwajiri.
 



Magari ya serikali ndiyo mzigo mkubwa kwa uchumi wa nchi yetu. Napenda kuishauri serikali ifanye mambo yafuatayo katika kudhibiti matumizi ya hovyo hovyo ya mali za Watanzania:-
  • Magari ya Serikali yatumike kwa kazi za kiserikali peke yake.
  • Magari ya Serikali yaegeshwe kwenye maegesho ya ofisi za serikali muda wa kazi unapofika isipokuwa kama kuna sababu maalum .
  • Watumishi wote wa wizara, mashirika na taasisi za serikali watumie magari yao binafsi wanapoenda kazini na kurudi nyumbani.Watumishi hawa hawalipi kodi wanapoingiza magari yao binafsi, pia mabenki yote yanatoa mikopo ya muda mrefu kwa watumishi hawa kwa dhamana ya ajira yao kama watumishi wa umma.
  • Viongozi wanaoweza kurudishwa nyumbani na kuchukuliwa asubuhi iwe ni kwa mawaziri, waziri mkuu, makamu wa raisi na rais peke yao. Wengine watumie usafiri wa umma au magari yao.
 
Hii ni big challenge kwa MAMA HAWA GHASIA, Waziri mwenye dhaman ya mishahara kwa Madereva na wafanyakazi wote wa sector ya umma.

JE, MISHAHARA INATOSHA KWA WAFANYAKAZI?????????????????
 

Mkuu MajiM..., hapo umegonga pale panapo penye kabisaaaa..... Unajua hapa nyumbani wafanyakazi wa Serikali hawalipi Kodi waingizapo magari lakini still tunawapa tena gari ya ofisi...... sasa ule msamaha wa kodi ni kwa manufaa gani??

Mimi nadhani inabidi tuangalie hizo pointi zako mbili muhimu hapo juu na kujaribu kujipanga kuelekea kwenye ufanisi.....
 
Ndugu wa Jamii forum, nimeshidwa kuleta nyeti zozote kwa mda mrefu kutokana na mambo mawili; kwanza sijaona jina lolote jenuine kwanye list ya members. Sijajua nini maana yake, na kwasababu mimi nilijiandikisha nikiwa nje ya nchi kuna vitu nilikuwa sivielewi saaana. Jambo la pili ni jinsi maada zilivyokuwa zikienda, kwangu niliona kama kuna-kucheza na hatari hasa kwa wakati huu ambapo vigogo wetu hawapendi kukosolewa. Mambo niliyotaka kufanya ni either kuondoa identity yangu halisi na kuwa kama 1. Invisible, 2. kikongwa, 3. Mzee wa kijijini etc.

That said, I would like you to provide some directives on how to edit some personal particulars in Jamii Forum. I hope there are many people who would like to contribute, especially those in the diaspora, but its a bit scary seeing that all members have nicknames.

Nataraji kupata maelekezo yenu
 
Geoffrey Barweta dereva anayemwendesha Mkurugenzi Mkuu wa EPZ kwa wanaomjua humuita "Kagame" inasemekana hata mazingira yake ya kuacha kazi jeshini ya utata na pia anahisiwa kuwa ni raia wa Rwanda (uraia wake una mashaka).

Pamoja na yote hayo magari ya serikali sasa yapewe amri ya kutekeleza agizo la kuyaandika Majina ya idara/wizara/taasisi ubavuni.

Hili litasaidia sana, vile vile utumiaji wa magari haya kwa shughuli binafsi umekithiri siku za kawaida hata weekend. Unaweza kukutana na gari la serikali asubuhi limebeba watoto wa bosi likiwapeleka shule wakiwa wao na dereva tu. Mamalaka sijui hazioni uozo huu? Hayo nayo ni matumizi ya ovyo sawa na kwenda kuibia gari la serikali.

 
Ni mmoja kati ya wengi hivyo hakuna haja ya kushangaa.
 
Hii thread mbona ni ya miaka mingi sana?????? Kweli watu waishiwa idea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…