Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,672
Niaje wanaJamiiForums?
Nimekutana na haya maeneo ambayo hayaelezeki historia yake na mengine maelezo yake hayana mashiko, lakini maeneo haya yana maajabu yake tofauti na chumba chako cha kulala.
1.AREA 51
Eneo hili lililo zaidi ya miles 80 nje ya jiji la Las Vegas limekuwa likitajwa kuwa ndipo yalipohifadhiwa mabaki ya Alien walioanguka mwaka 1947. Mpaka sasa hii ni kambi ya jeshi na kuna ulinzi mkali kuzuia raia na aina yoyote ya kiumbe ambacho hakijaruhusiwa kuingia katika eneo hilo.
Inasemekana jeshi la Marekani lilichukua teknolojia ya Alien lakini bado halijaanza kuitumia, huku wengine wakisema kwamba hakuna ushahidi wa kuwepo kwa mabaki ya Alien na kwamba ulinzi mkali katika eneo hilo ni kutokana na kwamba ni eneo la jeshi na ni lazima lilindwe.
2.BERMUDA TRIANGLE
Eneo hili la bahari linasemekana kumeza meli kubwa na ndogo pamoja na ndege na zisipatikane tena. Eneo hili liko magharibi mwa bahari ya Atlantic na ni moja kati ya maeneo ambayo yamehusishwa na stori za kusadikika, kiimani pamoja na wengine wakisema geography ya eneo hilo ndio husababisha kupoteza au kuzamisha vifaa hivi vya usafiri.
Kama ilivyo kwa walimwengu, pia eneo hili halikuachwa kuhusishwa na nguvu za Alien na kwamba hili ni eneo ambalo wameficha vitu vyao. All in all hili ni eneo hatari sana kwa vifaa kama ndege za abiria na binafsi, meli na vifaa vyote vya usafiri wa majini.
3.ATLANTIS CITY
Hili ni jiji linalosemekana kupotea baharini. Katika maandishi ya Plato mara mbili alielezea mji ambao ulikuwa mbele katika teknolojia lakini watu wake walikuwa ni wabaya na waliotaka kuitawala dunia kwa nguvu. Katika stori hii ya Plato aliandika kwamba baadhi ya viongozi na wana Atlantis wakongwe na wazawa waliupinga mpango huo kwa nguvu zote.
Mji huu umebaki historia isiyokuwa na mashiko, kwani wakati ambapo Plato ambaye ndiye aliyeanzisha uvumi huu alisema kwamba watu wa Atlantis hawakuwa na nia nzuri, lakini wataalam wamekuwa wakisema mji huo ulikuwa na watu wenye teknolojia ya juu na walikuwa na lengo zuri na jamii ya dunia.
4.PYRAMID EGYPT(MISRI)
Pamoaja na kwamba inawezekana ni moja kati ya picha maarufu sana ulimwenguni, Pyramid hizi bado zinaendelea kuwa za kipekee na ambazo mpaka sasa ujenzi wake haujaweza kuelezeka. moja kati ya vitu visivyoingia akilini ni pamoja na kwamba pyramid hizi zimejengwa takribani miaka 2589 BC na 2504 BC, na kuwa na urefu wa mita 481 bado hakuna anayeweza kusema kwa wakati huo waliwezaje kutumia mawe ya uzito wa tani mbili kujengea?
5.STONE HENGE
Mawe haya makubwa huko UK yameendelea kuwa na stori za kusadikika tu. Hakuna anayeweza kusema yaliwekwa kwa ajili ya kazi gani?
Wengine wamesema ni kwa ajili kujilinda na vipindi vya winter, wengine wamesema ni sehemu ya kutua kwa UFO japo hakuna linaloweza kuthibitishwa. Hakuna maandishi yoyote yaliyoachwa hapo na limekuwa eneo mojawapo zuri kwa ajili ya utalii huko UK.
All in all dunia ni sehemu yenye mambo mengin mazuri na maajabu mengi sana, vizazi na vizazi zimepita na kutuachia urithi wa maeneo haya na dunia hii tuitunze kwa ajili ya maisha ya vizazi vijavyo.
ifakara Baby