Shambulio la bomu Brussels, mtuhumiwa auawa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,604
2,000
Wanajeshi wa Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa muhanga, katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.

Idara ya polisi imesema kuwa mtu huyo alikuwa amevalia kile kilichoonekana kuwa mkanda wa vilipuzi na kuwa kulitokea mlipuko mdogo.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.

Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.

Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu mwaka uliopita kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi.bbc swahili
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,217
2,000
Kwa sasa ulaya imekuwa main target ya magaidi.Nchi kama ufaransa,uingereza,ujerumani na ubelgiji wamekuwa wahanga wakubwa
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,891
2,000
Acha Na Wenyewe Waishi Kama Libya Iraq Syria Kwa Sababu Wao Ndiyo Chanzo Cha Yote Kabla Hawajavamia Hizo Nchi Waarabu Waliishi Kwa Amani Kabisa Hapakuwahi Kuwa Na Wakimbizi Acha Waisome Namba Halafu Magaidi Hawajui Inatakiwa Waende Viwanja Vya Mpira Kama Pale Wembley Lipua Wote Waliomo Na Wenyewe Waone Uchungu Sishabikii Ugaidi Ila Kwa Hili La Wazungu Acha Watandikwe tu Hakuna Namna Wao Ndiyo Chanzo
 
havanna

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
1,740
2,000
Ukifanya mabaya kwa mwenzako usitegemee mazuri, hawa jamaa ndio wameleta vita, magonjwa na matatizo kedekede kwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu, nadhani ile tabia ya kupigana wenyewe kwa wenyewe imewachosha wameshagundua adui wao ni nani, yetu macho
 
1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,151
2,000
Kwa sasa ulaya imekuwa main target ya magaidi.Nchi kama ufaransa,uingereza,ujerumani na ubelgiji wamekuwa wahanga wakubwa

Ulaya wamejitakia wenyewe haya....waliunga mkono ugaidi huko Libya walipomwangusha Ghadafi...wakaunga mkono huko Afghanistani...huko Syria nako wakaunga mkono ugaidi dhidi ya serikali....Wakampindua Saddam Hussein wa Irak na kumuua kwa kuwasaidia wapinzani wa Saddam Hussein ...Yaani wazungu bure kabisa...wanaunga mkono vikundi hivyo vya ugaidi na kufifadhilii...Sasa mambo hayo yamewarudia wenyewe...Wakati anakufa Gadhafi alibashiri hivyo kwamba waliomwangusha wakiwemo wazungu watajuta....Sasa ugaidi umeingia huko ulaya...Maelfu ya wakimbizi wa Libya na Syria wamekimbilia huko ulaya...Wazungu hawakujua kuwa kwa kuiangusha serikali ya Libya na kuleta vurugu Syria, wakmbizi wangeanza kummiika ulaya....It was a blunder and still it is a blunder....Kinachotokea ulaya kwa sasa ni mwanzo tu wa makubwa zaidi yanayokuja au yatakayowafika hao wazungu....Can you imagine somewhere magaidi wanaandaa bomu la nyuklia??? Can you you imagine magaidi wakilipua mitambo ya nyuklia huko Europe au USA????
 
Hatari sana mkuu
 
Wgr30

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
1,728
2,000
Wacha na wenyewe waonje joto la jiwe, walipokuwa wanakimbizana kwenda mashariki ya kati na Afrika kasikazini kuonyesha siraha zao kana kwamba kuna tuzo huko hawakujua kwamba hata wanaopigwa ni binadamu!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom