Shamba shape up: Kipindi hiki hakiwezi kuonyesha wataalam wa Tz?

Hapo zamani kama sikosei walikuwa tz, na walitumia wataalamu wetu, uzuri wana record ya hivyo vipindi unaweza ona pitia website yao au youtube page yao, ikopoa sana, episodes zote zinapatikana
 
Hapo zamani kama sikosei walikuwa tz, na walitumia wataalamu wetu, uzuri wana record ya hivyo vipindi unaweza ona pitia website yao au youtube page yao, ikopoa sana, episodes zote zinapatikana
Samahani hoyo link au kipindi cha you yube kuona epsode zote naipataje
 
Habari za jioni,
Kuna kipindi kina kichwa cha habari hapo juu cha utv muda wa jioni ningependa kujua hivi kipindi hiki hakiwezi kuonyesha wataalam wa Tz waliopita SUA.
Washauri waliopita SUA waanzishe cha kwao hicho ni cha Wakenya! Binafsi ninakipenda. Presentation yao ni nzuri! Huko nyuma kupitia RTD tulukuwa na vipindi bomba zaidi japo TV zilikuwa bado. Mfano "Mkulima wa kisasa". Hata magazeti yake yalikuwepo na yaliandaliwa kwa series.
 
Kuna baadhi ya episodes walikuja Arusha na kuwatumia baadhi ya maafisa ugani wetu..ni kipindi kizuri sana kwa wakulima na wafugaji..
 
Washauri waliopita SUA waanzishe cha kwao hicho ni cha Wakenya! Binafsi ninakipenda. Presentation yao ni nzuri! Huko nyuma kupitia RTD tulukuwa na vipindi bomba zaidi japo TV zilikuwa bado. Mfano "Mkulima wa kisasa". Hata magazeti yake yalikuwepo na yaliandaliwa kwa series.
Yes, presentation na material content ni nzuri kwa walengwa, a clear message is delivered to the intended audience!
 
Yes, presentation na material content ni nzuri kwa walengwa, a clear message is delivered to the intended audience!
Hapa kwetu,kuna kitu hakiko sawa,tunaanzisha vitu vizuri,baadae tunavidharau,wenzetu wanavipick wanaboresha kidogo tuu. Nimeangalia scenery na motive yao,haipishani na kitu fulani TFA (Tanganyika Farmers Assosciation)ilikuwa ikifanya kwa wakulima na wafugaji huko nyuma enzi za GM Mr. Mshiu. Hivi sasa hata kama vipo,tunazidisha propaganda zaidi ya uhalisia. Nina mifano.
 
Taabu kila mtu mwanasiasa?wataalamu wa sua waliosomea kilimo na mifugo wako bize kwenye siasa badala ya proffesional zao
 
Habari za jioni,
Kuna kipindi kina kichwa cha habari hapo juu cha utv muda wa jioni ningependa kujua hivi kipindi hiki hakiwezi kuonyesha wataalam wa Tz waliopita SUA.
Umesema kitu ndugu! Hiki kipindi nakibahatishaga ITV sijui siku. Kwa kuwa napenda sana kilimo, sifaidi vizuri kwani mandhari ya kipindi ni Kenya.
Inashangaza kwamba pamoja na kuwepo kwa SUA na vyuo vingine vya kilimo hakuna anayejitokeza kuiga mfano wa hiki kipindi kuanzisha kingine kwa ajili ya specifically wakulima wa Tanzania.

Enyi wataalamu wa kilimo tanzania, mmelala au mmezubaa?
 
Hapa kwetu,kuna kitu hakiko sawa,tunaanzisha vitu vizuri,baadae tunavidharau,wenzetu wanavipick wanaboresha kidogo tuu. Nimeangalia scenery na motive yao,haipishani na kitu fulani TFA (Tanganyika Farmers Assosciation)ilikuwa ikifanya kwa wakulima na wafugaji huko nyuma enzi za GM Mr. Mshiu. Hivi sasa hata kama vipo,tunazidisha propaganda zaidi ya uhalisia. Nina mifano.
Nchi yetu haina vipaumbele na hatujui tunahitaji nini. Mafanikio huanzia chini mashinani na sio kuanzia na ndoto za viwanda huku wazalishaji wa malighafi hawajaandaliwa na wanunuzi wa bidhaa zinazotarajiwa kutengenezwa uwezo wao wa manunuzi unazidi kuporomoka.

Hivi vyuo vyetu vya Kilimo na Mifugo vipo tangu zamani sana, lkn tija inakosekana mashambani sababu hivi ni vyuo vya kupika MAAFISA KILIMO NA MIFUGO. Hatuna vyuo vya kupika WAKULIMA na WAFUGAJI.

Entry qualifications, aina za kozi na matarajio yaliyowekwa hayamgusi Mkulima Mtanzania kwa namna iliyopaswa. Hatuna kozi za wakulima, kuna kozi za maafisa kilimo ambao wakishahitimu wanakimbilia fani zingine.

Nafuu ya kilimo chetu tunayoiona imeletwa na TASAF na ule mpango wa SHAMBA DARASA na kuhamasisha utumiaji wa mbegu bora. Lakini vyuo ni sifuri. Tunajivunia usomi usio na manufaa badala ya kufundishana stadi za kazi mashambani.

Shamba Shape Up ni mfano wa kuigwa. Wenzetu wanahamasishana hadi kupima udongo ili kuongeza uhakika wa mavuno. Hapa kwetu tunalima 'sandakalawe', mwenye kupata apate, mwenye kukosa abebe msalaba wake.

Serikali yetu ina makelele yasiyo na tija kwa vijana. Wizarani kumejaa wanasiasa 'wazoefu' wa siasa wasio na mawazo mapya kiutendaji. Kampeni za misimu za ukaguzi wa pembejeo wa kisiasa, mkulima anapuliza dawa na bado mimea inaliwa, hana msaada zaidi ya kusimangwa kuwa ni mvivu.

Ingekuwa ni amri yangu, vyuoni vyetu vingekuwa na kozi zenye muundo wa Shamba shape up
 
Samahani hoyo link au kipindi cha you yube kuona epsode zote naipataje
Kaka, ni vizuri siku nyingine ukajipanua na kufanya research, inasikitisha kwamba sisi watz bado ni wazito kuingia internet na kutafuta kitu, ila kwa youtube link ni hii shambashapeup - YouTube, ila wana webiste yao inaitwa shambashapeup.com, kwenye link ya tv shows inaweza ona za east africa na kila series ya nchi husika.
 
Ni kipindi kinachotoa elimu nzuri sana kwenye kilimo na ufugaji..Ni cha kenya ila huwa wanatembeleaga mpaka TZ...Wataalamu wetu wanaweza kuja na cha kwao cha namna ile ila wasi-copy na ku-paste kama anavyofanya Mc Pilipili kwenye vichekesho vyake...
 
Kaka, ni vizuri siku nyingine ukajipanua na kufanya research, inasikitisha kwamba sisi watz bado ni wazito kuingia internet na kutafuta kitu, ila kwa youtube link ni hii shambashapeup - YouTube, ila wana webiste yao inaitwa shambashapeup.com, kwenye link ya tv shows inaweza ona za east africa na kila series ya nchi husika.
Hukuwa na sababu yoyote ya kumsimanga kabla ya kumpa hiyo link. Kumpa umefanya kwa hiari yako a.k.a kìherehere chako hajakulazimisha
 
Shamba shape up ni cha Kenya .... wataalamu wetu waamke wawe wabunifu watengeneze cha kwetu kwa mazingira yetu ya kibongo bongo.
 
Back
Top Bottom