Shamba la Urithi

Shamba la Urithi

The MoNA

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2014
Posts
4,264
Reaction score
10,503
Inaumiza kichwa sana kwani ukiwa nje huwezi kuona ya ndani (sio nje ya nchi) ..

15 ni namba iliyo leta miyegusho kwa Taifa .. lakini ilileta Nuru na mwanga kwa kizazi

Mengi ambayo yalishikiliwa na wachache sasa yakawa yanapenyeshwa kwetu kwa namna ya utofauti mkubwa ....

Katika picha ya ukutani haiwekwi picha kama picha ila kioo mbele kinacho Ruhusu Ile picha kuonekana
Nyuma picha karatasi na kitukigumu kidogo kiubao ama kibox ambacho huwezi kuona Ile karatasi iliyo na picha ..

20 ilikua namba ya mapinduzi ... Ambayo hakuna mizizi usingeteteleka hata ule mzizi mkuu ungeguswa kwa namna ya utofauti ...

Na ndipo mkulima akawaiwa kabla hajakamilisha adhimio lake ...

Lakin kwa kua Alisha pembua kiasi majani yaliyo uzunguka mti na kutifuatifua kidogo
Ikawa ni rahisi kwetu kujua walau mpangilio wa mizizi ilivyo ....

Lakin kwa kua hatuna elimu na mti huo bado hatukuweza kujua hiyo mizizi katika mpangilio wake ni ipi inafaa kukatwa mpaka kuufikia mzizi mkuu

21 ikatoa ushindi kwa mti kwani mkulima alipo Anza kuuendea akagongwa na nyoka akazongwa na nyuki pia nge na tandu hawakumwacha salama hivyo kwa kuwa wengi wetu ukulima tuliukataa hivyo shamba alienda mwenyewe na akakosa msaada maana hata alipo dhulika tulikua hatuna habri tulizipata baadaye kwa kusikia harufu mbaya inayo Toka shambani kuongezeka ...

Kwa kuwa shamba ni la urithi Sio rahisi kupotea lakin kuchezewa na kunufasha wengine ndio kinacho endelea sasa ... Na kwa hakika wanaendelea kupanda mazao ya muda mrefu ili kusudi tukilihitaji basi waseme tusubiri mazao yao yakomae ndipo tuanze kuwaza kulilima shamba letu .. . ..

Kwa hakika neno mniombee halikutafsiriwa na wengi wetu kwa maana lilikua nineno lililo onekana la ulaghai kwamaana Imani ya maombi kwetu imetoweka hivyo hatukuweza kujua kama ilikua ni lugha. Ya wahenga iliyo kua ikituasa jambo .....

Hata pale tulipo pata taarifa ya mkulima kupatikana akiwa mzoga basi kwa walio kua wametangulia kusafisha nyumba kwa ajili ya wageni wakasema kulikua na matunda mengi sana ambayo yalifaa kuajili wakulima wengine lakin pia hatukushituka Wala kulitafakari kwa mlengo mpya Bali wa ubinafsi na ukichaa wa kujimilikisha shamba ...

Sasa Yale mazo yote aliyo kua ameyaacha mkulima yamekomaa mavuno yanaenda kwa wasafisha nyumba sie tusijue kitu ...

Lakin ndio tunaambiwa ni msimu wa kilimo hivyo tutume pesa ya mbegu ....

Kile kikao Cha familia Cha 29 kiliingia dosari kwasababu wale wasafisha nyumba walituandalia mtego na kutujaazia Moshi ulio tulevya wakatupata kwa kutusukumia kwenye mabanda ya Simba ambao mwanzo walikua ni mbwa waangalizi wa mashamba na nyumba ...

Mpaka pale ambapo gari zetu pia zilitolewa upepo kwenye mataili na pump walificha wao ...

Kuna haja sasa kikao kinacho fata tusome nyumba yetu tena maana Ina mabadiliko makubwa kias wao wanaijua maana ndio waliyonibadilisha pasipo kusoma basi ni kubomoa itagharimu lakini kwa muda wote tulio kaa mjini viakiba vya kujenga kibanda kikatusitili

Lakini wale Simba wakishiba nyama ama wakiwa na ulaji wa nyama hawana habari na windo jipya ...

Sasa kwa kua hawajua harufu ya anaye wafuga wanaweza wakamla ikiwa tutawatos kwenye Ile minyororo yao ... Na na baada ya hapo warudi porin ...

Pale tulipo kosea ndipo tulipo patia ....

MAONI:
Umeeleza vyema sana.
Natumai standard iliyowekwa kwenye kikao hicho 29, imewafanya warithi wa shamba wagundue pamoja na uzubaifu wa wenye shamba, kuna kuamka kimantiki kwa asilimia kubwa juu ya umiliki wa shamba. Hii imeleta tanziko na pumbaziko hata warithi wa shamba wana hofu.

Sasa tusubiri makatibu watatujuza nini kwenye 9 na washirika wa namba hiyo endelevu. Japo wasimamizi wa shamba bado hawapo tayari kuwaachia wajukuu shamba nao waanze kujitegemea kwa kuliendeleza shamba hilo liwafae wao na wajao. Wajukuu nia njema ni kwa shamba lao liwafae wote.
--------------------
Kikubwa wajukuu wkikubali kulilima hakuna kinacho wazuia maana nyaraka zote zinawapa kibali Cha umiliki na uendelezaji wa shamba hilo ...

Isipo kua bado shamba Lina mazao ambayo kwa mtizamo si wao walipanda na hayana faida kwao isipo kua hasara zaidi kwani mazao hayo humaliza rutuba ya shamba.

Story from X (C&P).
 
Back
Top Bottom