Shamba la Miti ya Mbao linauzwa

Shamba la Miti ya Mbao linauzwa

majorbuyoya

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
1,828
Reaction score
568
Heshima kwenu wana JF,

Shamba la Miti aina ya
Pinus Patula (P. patula) yenye umri wa miaka 8 na ukubwa wa hekari 35 (hekta 14). Lipo Mkoa wa Iringa katika Wilaya ya Mufindi kijiji cha Mapanda kilichopo umbali wa Kilomita 120 kutoka Mafinga mjini.


Shamba limepandwa na kufuata taratibu zote za Kitaalam kuanzia hatua za awali za kuotesha miche katika bustani, kuandaa shamba, upandaji hadi Usimamizi wa shamba baada ya kupanda. Vile vile kuna usalama dhidi ya moto kutokana na eneo shamba lilipo.

Shamba limefanyiwa thining mara moja ambapo miti iliyokuwa dhaifu kwa ukuaji imeondolewa ili kuipa nafasi ile mizuri iweze kukua na kutanuka zaidi. Vile vile, miti imefanyiwa pruning (kupunguza matawi) hiihusaidia kuongeza thamani ya mti kipindi itakapofikia wakati wa kuvunwa kwaajili ya mbao sababu matawi yanapoachwa kukomaa husababisha makovu pale tawi linapokatika na kovu lile huingia hadi ndani ya mti ambapo hufanya mbao ipungue ubora na mvuto inapotengenezewa furniture.

Miti imepandwa kwa umbali wa mita 2.5 kati ya mti mmoja na mwingine na umbali kati ya mstari mmoja na mwingine ni mita 2.5 ambapo inakadiriwa hekari moja kuwa na miti 823 au hekta moja miti 1680 kabla ya kufanyika kwa zoezi la kupunguza miti yenye udhaifu (Thinning).

Bei yake ni Milioni 3.5 kwa hekari moja na bei hiyo ni kwa miti pamoja na ardhi yake, kama unahitaji uvune miti peke yake kisha uache ardhi kwa mwenye Shamba, bei inapungua. Kwa umri wa miaka 8 unaweza kuanza kuchana mbao.

Kwa mtu ambaye yupo serious kwaajili ya biashara ani-PM
 
Ekari ngapi na ni wapi?

.......Shamba la Miti aina ya Pinus Patula (P. patula) yenye umri wa miaka 8 na ukubwa wa hekari 35 (hekta 14). Lipo Mkoa wa Iringa katika Wilaya ya Mufindi kijiji cha Mapanda kilichopo umbali wa Kilomita 120 kutoka Mafinga mjini.
 
Back
Top Bottom