Shamba la bibi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamba la bibi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oba, Mar 25, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Siku za hivi karibuni kuna mambo yamenitisha sana;
  1. Eti kuna mgodi wa madini katika poli moja huko Kahama na raslimali kutoka huko zinabebwa directly kupitia uwanja wa ndege uliopo hapo mgodini bila mtu yeyote kufanya editing ya kipi kinatoka na kipi kinabaki.
  2. Eti mheshimiwa Rais na waziri mkuu wa Tz kwa pamoja wameshirikiana kuzuia sheria kuchukua mkondo wake kwa kumzuia waziri wa barabara kufanya kazi ambazo wenyewe ndo walimkabidhi.
  3. Eti kuna tujamaa wizarani tumeajir watu hewa na tumekusanya mabilioni ya pesa ya kuwalipa hao watu
  Hivi tuna viongozi wawajibikaji kweli?wenye uchungu na raslimali za nchi hii na maendeleo yake?Hivi ni lini tutakapopata viongozi waadilifu ili tuwafungulie mashtaka hawa akina Chiluba wetu?
  Kama madini mgodini kahama yanaibwa kwa staili hiyo, ni raslimali ngapi nchi nzima ambazo zinachukuliwa kutoka kwenye shamba hili la bibi lisilo na mwenyewe?
  Viongozi wetu wataacha lini kufanya maamzi yenye ubnafsi wa kujilinda wao na watu wao? eti usivunje nyumba hizo kwani ukifanya hivyo kuna watu itabidi niwawajibishe kwa kutoa vibali vya ujenzi na mimi sipo tayari kufanya hivyo kwasababu ni watu wangu wa karibu?
  Eti waache hao wawekezaji wabebe mali zetu kwani ndo wamenifikisha hapa, hujui, huenda ndio walionisapoti kifedha nikapata nafasi hii, au wameahidi kunihifadhi mambo yakigeuka kwangu, au nina mgao na mimi katika mali wanazohamisha!
  Unamuajiri mtu chini ya Ofisi ya raaisi anafanya blanda na kupoteza mabilioni ya pesa na bado unamtuma surbodinate wako achukue hatua ambayo tayar ameshindwa kufanya hivyo na ndo maana umepata taarifa, are you real serious na mali za nchi hii? kwa nini usitumie madaraka yako kama mkuu uwadhibiti hao wahuni? Mwl Nyerere anapendwa mpaka leo kwa kuwa alikuwa na udikteta usio na ubnafsi bali kwa maslahi ya umma; watu kama hao angeweza kuwapoteza bila hat kulalamika kwenye vyombo vya habari kama wewe.
  Siasa ni ngumu, si muda mrefu wale wanaodhani kuwa na kinga watashangaa tunawapandisha kizimbani kwa wizi au kushindwa kuwajibika.
   
Loading...