Shall we?

Shall we?

SirAlfred006

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2020
Posts
552
Reaction score
1,306
Haujengwi kwa mbao!

IMG_20210928_090336.jpg
 
Umenikumbusha stori moja ya kwenye Gazeti la SANI. Lodi Lofa akawa ametembelaea studio siku moja, halafu akawa amepewa na watangazaji studio, nafasi ya kutuma salaam pamoja na kuwapa ujumbe wale aliokuwa anawatumia salaam. Lodi Lofa akafanya hivyo, akataja list ya majina ya watu kadhaa akawatumia salaam na mwisho akasema "ujumbe: mtu chake"
Baada ya hapo tena akapewa nafasi nyingine ya kuchagua muziki ili uchezwe studio, akaulizwa swali "baada ya kutuma salaam, unaweza kuchagua sahani yoyote ya kukuburudisha?" Lodi Lofa akajibu "sahani moja tu ya pilau iliyoshindiliwa barabara itanitosha"
Kwa kipindi hicho, sahani au kwa jina jingine santuri, zilikuwa ni kana CD zenye umbo kubwa zilizokuwa zinahifadhi muziki na kuchezwa kwa kutumia vifaa vilivyokuwa vinaitwa Record Player.
Watangazaji studio walimaanisha sahani ya muziki, Lodi Lofa yeye akili yake ikawa imekimbilia kwenye chakula, japo hata sahani za muziki alikuwa anazifahamu
 
Back
Top Bottom