Shaka (CCM) uso kwa uso na Freeman Mbowe (CHADEMA) kwenye Msiba wa Baregu, Rais Samia atoa Chozi

du
 
Nawapa pole wafiwa na wapenda demokrasia wote.

Nawapongeza CCM kwa uungwana na kupeleka ujumbe mzuri kwa Watanzania.

Utofauti wa vyama ni ziada, kilicho muhimu kuliko vyote, ni utanzania wetu. Tuuenzi Utanzania wetu, kama ingekuwa inawezekana, tungependa nchi nyingine waje kujifunza siasa za kistaarabu kutoka kwetu. Ni bahati mbaya, kuna wajinga wachache wanaoona fahari kuendekeza siasa za kibaguzi.

Mungu wetu uzidi kutujalia hekima maana wewe ni mwingi wa hekima. Utujalie hekima ya kupendana bila unafiki. Mama Samia na Shaka, Mbowe na viongozi wengine wa vyama vyote vya siasa, Mungu awajalie hekima ili ninyi muwe ndiyo sababu ya utengamano badala ya mafarakano.
 
Miezi mitatu ni mingi sana kwenye maisha..... Shaka alikuwa benchi akituhumiwa kuchukua rushwa akiwa katibu wa CCM Morogoro wakati wa uchaguzi wa Meya. Angekuwepo Bwana Jiwe, Polepole asingetia mguu hapa.
 
Jamaa mboye si alisema ameshapata chanjo sasa barakoa ya nn
Kupata chanjo haina maana usivae barakoa .

Unaweza ukawa na virusi vya korona huku ukiwa na chanjo na visikuathiri wewe na vikawaathiri wengine ukawasambazia
 
..mwingine alikuwa mbinafsi kila wakati alitaka aombewe yeye tu.

..hata kwenye misiba alilazimisha waliofiwa wamuombee yeye binafsi badala ya kuombea marehemu wao.
 
Mkuu huyo mvuta uzi, anamaana Rais Samia katuma ujumbe kwenye ulioongozwa na Katibu Mwenezi wa CCM Shaka, basi suala la kutokwa na Chozi ni la SHAKA.
Kwahio aliyetoa chozi ni Shaka na sio Samia ? Duh basi hii lugha yetu ya Taifa ni ngumu sana wewe hii sentensi ungeielewa vipi ?

shaka-ccm-uso-kwa-uso-na-freeman-mbowe-chadema-kwenye-msiba-wa-baregu-rais-samia-atoa-chozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…