Shaka (CCM) uso kwa uso na Freeman Mbowe (CHADEMA) kwenye Msiba wa Baregu, Rais Samia atoa Chozi

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
CCM YAMUAGA PROF BAREGU

Familia wamshukuru Rais SAMIA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshiriki ibada ya kuaga mwili wa Profesa Mwesiga Laurent Baregu iliyofanyika usharika wa KKKT Kunduchi Beach, Dar es Salaam Ijumaa 18 Juni 2021.

"Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaja Prof Mwesiga Baregu kuwa alikuwa ni mwanazuoni mzalendo, aliyetumia taaluma yake katika kuimarisha na kuhuisha demokrasia nchini na ni mwanasiasa nguli aliyependa siasa safi na siasa za hoja kwa ustawi wa watanzania, daima tutamkumbuka na kuenzi."

Alisema Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akiwasilisha salam za Rambirambi.

Msemaji wa Familia hiyo Prof Kaijage amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa kiungwana kwa kuwa nao katika kipindi chote cha msiba na maombelezo ya mpendwa wao.

"Rais Samia ametufariji sana wote mlisikia kupitia Vyombo vya Habari na mitandao baada msiba huu kutokea alitufariji, kwa salam za pole na leo amemtuma mwakilishi wake ametupa nguvu na tunathamini sana hili kwa kuwa tumekuwa nae katika kipindi hiki kigumu kwetu wanafamilia " Prof Kaijage.

Prof Baregu amesafirishwa leo kuenda nyumbani kwao Mkoani Kagera kwa Mazishi.

MY TAKE:

Barakoa ina kazi gani? Au changa la macho? Corona ipo.

IMG-20210618-WA0029.jpg
IMG-20210618-WA0030.jpg
IMG-20210618-WA0031.jpg
IMG-20210618-WA0028.jpg
IMG-20210618-WA0027.jpg
IMG-20210618-WA0026.jpg

IMG-20210618-WA0025.jpg

IMG-20210618-WA0024.jpg
 
Ahhh chozi litoke wapi! Pengine kaja kushuhudia kweli kama kafa' mmoja wa kwenye kambi ya mahasimu wao wakubwa.
Huenda ni kweli chozi limetoka na Marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika Taifa hili (hilo sibishi), pia nadhani walikuwa nae kwenye Tume ya Katiba.

Issue yangu sijamuelewa aliyeleta hii habari au huenda kaileta vibaya..., heading inasema chozi limetoka alafu content inasema alituma mwakilishi...., sasa sikuelewa kama hilo chozi alilituma kwenye Risala.

Nimehoji tu ili niweze kuelewa
 
Huenda ni kweli chozi limetoka na Marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika Taifa hili (hilo sibishi), pia nadhani walikuwa nae kwenye Tume ya Katiba...,

Issue yangu sijamuelewa aliyeleta hii habari au huenda kaileta vibaya..., heading inasema chozi limetoka alafu content inasema alituma mwakilishi...., sasa sikuelewa kama hilo chozi alilituma kwenye Risala...

Nimehoji tu ili niweze kuelewa
Mkuu huyo mvuta uzi, anamaana Rais Samia katuma ujumbe kwenye ulioongozwa na Katibu Mwenezi wa CCM Shaka, basi suala la kutokwa na Chozi ni la SHAKA.
 
Huenda ni kweli chozi limetoka na Marehemu alikuwa na mchango mkubwa katika Taifa hili (hilo sibishi), pia nadhani walikuwa nae kwenye Tume ya Katiba...,

Issue yangu sijamuelewa aliyeleta hii habari au huenda kaileta vibaya..., heading inasema chozi limetoka alafu content inasema alituma mwakilishi...., sasa sikuelewa kama hilo chozi alilituma kwenye Risala...

Nimehoji tu ili niweze kuelewa
Ahahahahahahaha mkuu!
 
Back
Top Bottom