Shaka (CCM) uso kwa uso na Freeman Mbowe (CHADEMA) kwenye Msiba wa Baregu, Rais Samia atoa Chozi

CCM YAMUAGA PROF BAREGU

Familia wamshukuru Rais SAMIA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshiriki ibada ya kuaga mwili wa Profesa Mwesiga Laurent Baregu iliyofanyika usharika wa KKKT Kunduchi Beach, Dar es Salaam Ijumaa 18 Juni 2021.

"Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaja Prof Mwesiga Baregu kuwa alikuwa ni mwanazuoni mzalendo, aliyetumia taaluma yake katika kuimarisha na kuhuisha demokrasia nchini na ni mwanasiasa nguli aliyependa siasa safi na siasa za hoja kwa ustawi wa watanzania, daima tutamkumbuka na kuenzi."

Alisema Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akiwasilisha salam za Rambirambi.

Msemaji wa Familia hiyo Prof Kaijage amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa kiungwana kwa kuwa nao katika kipindi chote cha msiba na maombelezo ya mpendwa wao.

"Rais Samia ametufariji sana wote mlisikia kupitia Vyombo vya Habari na mitandao baada msiba huu kutokea alitufariji, kwa salam za pole na leo amemtuma mwakilishi wake ametupa nguvu na tunathamini sana hili kwa kuwa tumekuwa nae katika kipindi hiki kigumu kwetu wanafamilia " Prof Kaijage.

Prof Baregu amesafirishwa leo kuenda nyumbani kwao Mkoani Kagera kwa Mazishi.

MY TAKE:

Barakoa ina kazi gani? Au changa la macho? Corona ipo.
View attachment 1822954View attachment 1822955View attachment 1822956View attachment 1822957View attachment 1822958View attachment 1822959

View attachment 1822960

View attachment 1822961
du
 
Nawapa pole wafiwa na wapenda demokrasia wote.

Nawapongeza CCM kwa uungwana na kupeleka ujumbe mzuri kwa Watanzania.

Utofauti wa vyama ni ziada, kilicho muhimu kuliko vyote, ni utanzania wetu. Tuuenzi Utanzania wetu, kama ingekuwa inawezekana, tungependa nchi nyingine waje kujifunza siasa za kistaarabu kutoka kwetu. Ni bahati mbaya, kuna wajinga wachache wanaoona fahari kuendekeza siasa za kibaguzi.

Mungu wetu uzidi kutujalia hekima maana wewe ni mwingi wa hekima. Utujalie hekima ya kupendana bila unafiki. Mama Samia na Shaka, Mbowe na viongozi wengine wa vyama vyote vya siasa, Mungu awajalie hekima ili ninyi muwe ndiyo sababu ya utengamano badala ya mafarakano.
 
Miezi mitatu ni mingi sana kwenye maisha..... Shaka alikuwa benchi akituhumiwa kuchukua rushwa akiwa katibu wa CCM Morogoro wakati wa uchaguzi wa Meya. Angekuwepo Bwana Jiwe, Polepole asingetia mguu hapa.
 
..mwingine alikuwa mbinafsi kila wakati alitaka aombewe yeye tu.

..hata kwenye misiba alilazimisha waliofiwa wamuombee yeye binafsi badala ya kuombea marehemu wao.
 
Mkuu huyo mvuta uzi, anamaana Rais Samia katuma ujumbe kwenye ulioongozwa na Katibu Mwenezi wa CCM Shaka, basi suala la kutokwa na Chozi ni la SHAKA.
Kwahio aliyetoa chozi ni Shaka na sio Samia ? Duh basi hii lugha yetu ya Taifa ni ngumu sana wewe hii sentensi ungeielewa vipi ?

shaka-ccm-uso-kwa-uso-na-freeman-mbowe-chadema-kwenye-msiba-wa-baregu-rais-samia-atoa-chozi
 
Back
Top Bottom