Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,420
- 33,982
LEO SIKU YA KUZALIWA SIJALI ADAM SIJAONA
Rafiki yangu Sijali Adam Lawi Nangwanda Sijaona kaniletea ukurasa mmoja wa shajara ya baba yake marehemu Mzee Lawi Nangwanda Sijaona ambayo aliandika, ‘’Baby boy is born at 4 pm.’’
Huyu mtoto ni Sijali Sijaona na tarehe yake ya kuzaliwa ni leo 20 June, 1955.
Mimi nilimjua Sijali kupitia Abubakar Kirundu katika miaka ya 1970 sote watoto na tukawa marafiki tukikutana tunazungumza.
Tukapoteana kwa miaka mingi tumekuja kukutana tena sasa sote watu wazima na kilichotukutanisha ni mapenzi yetu katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Sijaona ameacha historia nzima ya maisha yake katika maandishi na nyaraka maandishi na nyaraka ambazo zenyewe kwa kujitegemea bila ya sisi kuongeza chochote ni historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Picha ya zamani kabisa niliyokuwanayo ya Mzee Sijaona ni picha iliyopigwa mwaka wa 1956 Ukumbi wa Arnautoglo ukimwonyesha yeye, Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz wakiwa katika dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO.
Picha hii alinipa Kleist Abdul Sykes.
Sijali Sijaona ana mengi sana kuhusu baba yake kwa maneno na kwa nyaraka na picha.
Nyaraka za Lawi Nangwanda Sijaona zinashindana na Nyaraka za Sykes.
Sijali ameniletea nyaraka nyingi sana za baba yake.
Lawi Sijaona ameacha shajara ambazo zinaweza zikasomwa bila ya shida tofauti na shajara za Abdul Sykes ambazo baadhi aliziandika kwa ‘’short hand,’’ yaani hati mkato.
Hizi shajara hazisomeki kirahisi.
Siku Sijali alipotembelea Maktaba nilimshawishi tufanye kipindi cha marehemu baba yetu na alinikubalia.
Video hii imependwa sana na imetizamwa hadi sasa baada ya miezi tisa na watu 12,000.
Ndugu zanguni iangalieni hii video muijue historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Happy Birthday Sijali.
Mungu akupe afya na umri mrefu.
View: https://youtu.be/82xOyiMkHJQ?si=tPjf74_Gf9pmSy22