Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,067
- 1,425
Walimwengu ndo wabaya
Jama nipo mahututi, tena ndani icuu
Mekurubia mauti, nahema kwa juu juu
Siwezi swali kunuti, Mola anipe nafuu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Wamenipiga ulozi, ule wa chuo kikuu
Kwa uchanga kimalezi, sijafikia wakuu
Nipo mbali na wazazi, kwa mamita elfuu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Mniombee na dua, ili iwe asibabu
Haya ninayo ugua, yeye ndo wa kunitibu
Msidhani ni mafua, nikaenda kama dubu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Abuuabdillah ✍️
0744 883 353
Jama nipo mahututi, tena ndani icuu
Mekurubia mauti, nahema kwa juu juu
Siwezi swali kunuti, Mola anipe nafuu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Wamenipiga ulozi, ule wa chuo kikuu
Kwa uchanga kimalezi, sijafikia wakuu
Nipo mbali na wazazi, kwa mamita elfuu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Mniombee na dua, ili iwe asibabu
Haya ninayo ugua, yeye ndo wa kunitibu
Msidhani ni mafua, nikaenda kama dubu
Dunia haina baya, walimwengu ndo wabaya
Abuuabdillah ✍️
0744 883 353