Shairi: Mapenzi pasipo pesa

Shairi: Mapenzi pasipo pesa

Tamu3

Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
28
Reaction score
18
MAPENZI BWANA NI PESA

Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena,
Ukiwa na nyingi pesa, tapendwa na wasichana,
Macho kwako tapepesa, hela wakishaziona,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.

Babu wa myaka tisini, apendwa na wasichana,
Unajua ni kwanini, waulizwe wasichana,
Pesa wanazitakeni, wende gauni kushona,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.

Uzee hawatojali, wanakijali kibunda,
Wanataka mwenye mali, huyo ndiye wampenda,
Kwake hawana kauli, wanamkabidhi tunda,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.

Binti hasa wa mjini, anavipenda vibabu,
Adai vina madini, almasi na dhahabu,
Wana Hela mfukoni, kutoa hawana
ta'bu,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.

Binti hao wa mjini, hawawataki wakaka,
Wadai si walaini, kiombwa pesa waruka,
Au dau lao chini, halitotosha kusuka,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.

Ukishakuwa na hela, binti wapanga foleni,
Kwako wataka kulala, mwilini wadungwe pini,
Wataka pewe chakula, cha sebule na sirini,
Mapenzi bwana ni pesa, wahenga walishanena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom