Shairi la Saa ya Ukombozi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,492
4,770
SAA YA UKOMBOZI.

1)Watu watakuwa huru,haki itapatikana.
Utatoweka udhuru,wao watapotengana.
Tuwe wakali ka faru,kwa umoja kushikana.
Ni saa ya ukombozi,karibia inafika.

2)Natushikane mikono,tusiwaze kutengana.
Tuyaache malumbano,adui ashindwe kunena.
Tutende yetu maono,ya usiku na mchana.
Ni saa ya ukombozi,karibia itafika.

3)Tusidhani ni rahisi,vita hivi kupigana.
Uchungu tutauhisi,japo tutalia sana.
Tupambaneni kwa kasi,tusiogope vijana.
Ni saa ya ukombozi,karibia itafika.

4)tuloyasema ni mengi,myaka ile hadi jana.
Tumefanya mbinu nyingi,kwa juhudi kukazana.
Zimekumbwa na vigingi,ya mwisho ni kupambana.
Ni saa ya ukombozi,karibia itafika.

5)Uoga tupunguzeni,tutende pia kunena.
Ujasiri tuvaeni,tupambane na mabwana.
Vita hivi tushindeni,mikono tukishindana.
Ni saa ya ukombozi,karibia itafika.
Shairi=SAA YA UKOMBOZI
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Kichwa kiwe "ndoto"?

Similar Discussions

Back
Top Bottom