Elimu ya kizamani, iliwajaza makupe,
Wakatunyonya jamani, tukabakia weupe,
Sasa tusiithamini, mashimoni tuitupe
ELIMU YETU YA SASA, YAWAFAA WATU WOTE.
Chako ni chako jamani, usikionee haya,
Sina nia kulaani, Elimu toka ulaya,
Bali natoa maoni, na tena bila ubaya,
ELIMU YETU YA SASA, YAWAFAA WATU WOTE.
Elimu ya kizamani, ilijaa ubaguzi,
Rangu walithamini, wakasahau ujuzi,
Sasa hayo hatuyaoni, tumetoa uchafuzi,
ELIMU YETU YA SASA, YAWAFAA WATU WOTE
Iondoe ubwana, Elimu ya Tanzania,
Watu kuitwa watwana, Aibu gani kisia,
Tuko sawa wote wana, Si Zuberi na Rukia
ELIMU YETU YA SASA, YAWAFAA WATU WOTE