Shairi: Dua Kwenu Marehemu

Mar 29, 2013
7
45
Anzali tulomo humu,waja wote tulobaki
Twaomba kwa ufahamu,kheri kwenu losabiki
Wapiganaji kaumu,walumbi wa taufiki
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Swala zetu zi muhimu,na mola aziafiki
Aifikiri sehemu,nzuri mkae lahiki
Mjaliwe maasumu,pumziko maburuki
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Niwape zenu salamu,kwa vyeo nisidhihaki
Wanasheria walimu,waandishi wa mikuki
Wachungaji maimamu,na wengine mashabiki
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Mlitumia kalamu,kutia ari mithaki
Mkafunga na swaumu,hiari yake riziki
Ikawapenya hukumu,chanzoke cha kisa hiki
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Ijapo mwanzo mgumu,vita mliimiliki
Kwa nguvu zilohishimu, nguvu za kiatomiki
Mkafa vifo vya damu,vifo vimetupa kiki
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Tumewachonga sanamu,wapenzi wetu ashiki
Enzi na enzi mdumu,vile mlivyojinaki
Sumu yenu sumsumu, alhamdullilahi
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki


Mwisho natia hanjamu,mtunzi nimehamaki
Karibuni wenye hamu,mzame kwenye handaki
Muonje chungu na tamu,kuteta na wenye chuki,
Dua kwenu marehemu,mlofia zetu haki

Innocent Zephania(Mnyika)
+255756680871
Kijenge-Arusha,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Similar Discussions

Top Bottom