Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
BODABODA.
1)imerahisisha kazi,watu twawahi kazini.
Masika na kiangazi,twapita barabarani.
Japo watutisha wezi,kuweka mawe njiani.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
2)buku pia hata jero,utafikishwa nyumbani.
Ila usione kero,vumbi likenda machoni.
Hata maasai yero,nae analo bomani.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
3)mengi utayaepuka,kama ukiwa makini.
Viunzi utaviruka,dereva ukijamini.
Epuka kukurupuka,usingie ajalini.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
4)wakwepa msongamano,chunga usipige chini.
Yakazuka malumbano,mwenye kosa ndio nani.
Usifanye mashindano,utashia kituoni.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
5)bodaboda si bajaji,taksi haina thamani.
Usilete ujuaji,utetanda lala wodini.
Washa huku ukijaji,waza fikiri makini.
Bodaboda gari langu,imekuwa msaada.
Shairi=BODABODA.
Mtunzi=Idd Ninga wa aTengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebool page=Idd ninga mashairi.
1)imerahisisha kazi,watu twawahi kazini.
Masika na kiangazi,twapita barabarani.
Japo watutisha wezi,kuweka mawe njiani.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
2)buku pia hata jero,utafikishwa nyumbani.
Ila usione kero,vumbi likenda machoni.
Hata maasai yero,nae analo bomani.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
3)mengi utayaepuka,kama ukiwa makini.
Viunzi utaviruka,dereva ukijamini.
Epuka kukurupuka,usingie ajalini.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
4)wakwepa msongamano,chunga usipige chini.
Yakazuka malumbano,mwenye kosa ndio nani.
Usifanye mashindano,utashia kituoni.
Bodaboda gari langu,japokuwa la hatari.
5)bodaboda si bajaji,taksi haina thamani.
Usilete ujuaji,utetanda lala wodini.
Washa huku ukijaji,waza fikiri makini.
Bodaboda gari langu,imekuwa msaada.
Shairi=BODABODA.
Mtunzi=Idd Ninga wa aTengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebool page=Idd ninga mashairi.