Yapendeza muoane.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
YAPENDEZA MUOANE.


1)Nimekaona kapicha,cha bibi na bwana yule
Leo sitaki kuficha,picha nimeona kule
Karembo kamejificha,siyo katoto cha shule
Ninga nakupa salamu,Uhega nenda uoe.


2)Mbona mnapendezea,funge pingu za milele
Siri nakudokezea,siseme kwa makelele
Mke nenda jiolea,watu tukupe kongole
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


3)Muitwe bibi na bwana,na posa mtoleane
Yapendeza kuungana,kwa harusi muoane
Siyo mje chezeana,kisha mje muachane
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


4)Uhega funguka kaka,mwambie Jina ukweli
Acha zunguka zunguka,kama waendesha meli
Wenzako wakimdaka,sije watia kabali
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


5)Hivi kuna shida gani,nyote mkikaa chini
Myafungue ya ndani,mpeane ya moyoni
Ama mwamwogopa Nani,kwanza hebu jaribuni
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


6)Jina mbona ni mahiri,tena ni mchapa kazi
Hadi natunga shairi,mengi nimeona wazi
Mbona haitaji gari,wala shamba la minazi
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


7)Voyota tutajichanga,hadi harusi ifungwe
Hata sasa najipanga,jinsi ya kufanya shangwe
Binti wa Watu mchanga,oa mikono ipungwe
Nyote mnapendezea,na yafaa muoane.


SHAIRI-YAFAA MUOANE
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
 
Back
Top Bottom