Shaibu wa miaka 76 ajinyonga kwa msongo wa mawazo

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mzee anayenufaika na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tasaf, Anthony Mikami (76) amejinyonga kwa kamba ya chandarua katika kijiji cha Nyabihanga kata ya Bukiriro wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kile kinachodaiwa kuwa na msongo wa mawazo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabihanga, Eradius Batakanwa amesema mzee huyo alijinyonga kwa kujitundika kamba kwenye mti mbali na makazi ya watu na aligundulika jana Jumatano Oktoba 24, 2018 saa 9:30 mchana kwa waliokwenda mabondeni kuvuna maharage.

Batakanwa amesema siku za hivi karibuni wakati wa uhai wake akiwa mnufaika wa Tasaf kijijini humo aliunguliwa na nyumba wakati akichoma viroboto na kuiteketeza nyumba hiyo.

"Baada ya kuunguliwa nyumba alichanganyikiwa maana alikuwa hana chakula cha usiku na mchana huku akiwa hana wasaidizi licha ya kujaliwa watoto watano wa kiume mmoja na wakike wanne," amesema Batakanwa na kuongeza kuwa hilo ni tukio la pili baada ya lile la kwanza lililotokea Februari.

Batakanwa pia amewataka watu wenye msongo wa mawazo kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini ili kuepuka kujiondoa uhai wao.

Mkuu wa kituo kidogo cha polisi kata ya Bugarama, Dotto Baraka na mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bukiriro, Themistocles Rubangula wamethibitisha kifo cha mzee huyo.
 
Afadhali alikuwa amekula chumvi,but ingekuwa kijana nguvu kazi ya taifa daaaaah ingekuwa sooo sad& disappointed
 
Jamaniii kama vijana tujitahd kukumbuka nyumbanii hata kwa kidogo tunacho pata kwanii kurudisha shukrani kwa wazazi wetu humfanya Mungu kutufungulia milango ya baraka zaidi tusiangalie nini wazazi wetu walitufanyia kiwe kizuri au kibayaa tusikae na vinyongo moyoni R.I.P Mzee😢😢🙏
 
Back
Top Bottom