Shahada 4 vs. Akili ya kuzaliwa

Jambo la msingi hapa ni hili: akili ni nini?

Kila mtu ana akili. Kile kinachoweza kuwa manufaa ya akili huitwa maarifa.

Aliye na maarifa ni pia mwenye elimu. Lakini mwenye elimu anaweza asiwe na maarifa.
 
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Alisema hivi: Akili ni kile unachobaki nacho baada ya kuwa umepoteza mchanganuo wote wa baadhi tu ya yale uliyowahi kufundishwa
Hapa hamaanishi kuwa "baada ya kuwa umepoteza mchanganuo wote wa yale yote uliyowahi kufundishwa, hapana". Ni baada ya kuwa umepoteza mchanganuo wote wa baadhi tu ya yale uliyowahi kufundishwa
Ukipoteza yote uliyofundishwa maana yake unakuwa kichaa ambaye hana memory, kwa sababu essentially yote uliyonayo kwenye ubongo ni ya kujifunza, na hivyo umefundishwa. Hata kama ulijifunza wewe mwenyewe, inamaanisha akili yako imeyatunza kama mambo uliyowahi kuifundishwa, kwa hiyo wewe kama wewe umefundishwa hata kwa yale ambayo uliwahi kujifunza mwenyewe, ubongo wako umeyatunza hivyo. Ukipoteza chote ilichofundishwa maana yake unapoteza memory yote, unakuwa binadamu kwa umbo tu ila kwa akli ni kitu kingine, almost alive dead!

Education is what is left after all the details are lost! ...... and not after all the education is lost
 
Huu uzi ndo nauona leo, jamaa alifunga kamba watu eti Newton hakwenda shule😂😂😂 wakati Newton kasoma chuo Cambridge university nakamaliza, pia eti Mark Zuck alikuwa kilaza ni uongo mtu mara hakusoma ,Mark alipiga shule baada ya shule kumsaidia kuvumbua Facebook akaona atumie muda wake huko maana tayari elimu imemkomboa , kitu sawa tu na Bill gates, watu wasiwachulie poa watu walio droup out from schools
 
Intellect sio akili mkuu.
Pia hakuna mtu ambaye hana akili
 
akili ni gari na elimu ndiyo dereva, sasa poteza vyote ulivyosoma na udhani kwamba utaendelea kutambua maandishi na kuyaandika Kama unavyofanya saivi hapa jf
 
Huku kwetu, maboss wote wameishia 4-kushaka chini Na kwenye mishe zao wanaajiri walio soma, ko kwenye hilo siwezi kubisha, Na wewe ulie sema wasio soma ndo vibarua, pole yako kaka
 
Alisema education is what remains after one has forgotten what has learned from school
Kwanza nnashindwa kuelewa mpaka hapo kuna uhusiano gani kati ya education na akili mleta mada
Tuanzie hapo alafu ngoja niendelee kusoma zaidi
 

Wewe endeleza upuuzi wako wa kupotosha jamii na usipeleke watoto shule

Kwa taarifa yako galileo alisomea pisa university
Mack Zuckerberg alisomea havard university ali drop out japo baadae walimtunuku honour degree

Newton na yeye alisoma pia na kuhitimu juu plus degree 1665
Galileo the same na yeye pia amesomea pisa university

Sasa wewe usisome utegemee kuna akili za kuzaliwa
Alafu kutokumaliza chu haina maana ya kwamba ndio nini labda hayo ni maamuzi binafsi ya mtu kutokana na ufanisi wake wa kufanya utatuzi wa mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…