Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,023
- 13,370
VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom, Azam FC, jana walizidi kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo, baada ya kuwalazimisha mabingwa watetezi Yanga sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku jinamizi la kukosa penalti likizidi kuwaandama Wanajangwani hao.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali, ilishuhudiwa Hamis Kiiza akikosa penalti muhimu ambayo huenda ingewapa pointi tatu muhimu na kupunguza uwiano wa pointi na vinara hao wa Ligi Kuu. Hii imekuja ikiwa ni takriban wiki moja na ushei, Said Bahanuzi alipokosa penalti muhimu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri.
Katika mchezo wa jana, Yanga walijipatia bao lao dakika ya 14, likifungwa na Didier Kavumbagu, akimalizia mpira uliotemwa na Kipa Aishi Manula, baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa Azam FC.
Azam walijibu dakika ya 22, lakini shuti la Kipre Tchetche liligonga mwamba kabla ya Kipa Manula kuokoa mchomo wa Emmanuel Okwi dakika ya 30. Dakika ya 35, Kocha Hans Van Puiljim alionekana akimlalamikia mwamuzi, Hashim Abdallah.
Hadi Mwamuzi Hashim Abdallah akipuliza filimbi kuashiria mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kabla ya kuanza, nyavu katika lango la Azam ziliachia na kutaka kuanguka, jambo lililomlazimu mwamuzi Abdallah kuanza kuzifunga akisaidiana na wachezaji, ambako David Mwantika, alipanda juu kuziweka sawa.
Yanga walianza kipindi hicho kwa kasi na dakika ya 58, Okwi alishindwa kutumia nafasi ya kufunga, baada ya Kipa Manula kuanguka na shuti lake kupaa, kabla ya dakika ya 60, Hamis Kiiza, kushindwa kuitendea haki krosi ya Joshua na kichwa chake kutoka nje.
Dakika ya 69, Yanga walipata penalti baada ya Erasto Nyoni kuunawa mpira eneo la hatari, lakini mkwaju wa Kiiza ulichezwa na Kipa Manula. Kutokana na kosa hilo, Nyoni alilimwa kadi nyekundu baada ya kupewa ya pili ya njano.
Alikuwa ni mtokea benchi, Kelvin Friday, dakika ya 83, alipoisawazishia Azam bao kwa shuti kali nje ya 18 na kumshinda kipa Juma Kaseja. Bao hilo liliwaamsha mashabiki wa Azam na wale wa Simba na kuanza kuimba CCM…CCM…CCM…
Hii ni sare ya pili mfululizo kwa Yanga, baada ya Jumamosi iliyopita kung'ang'aniwa sare tasa na Mtibwa Sugar mjini Morogoro, huku Azam ikitoka kuichabanga Coastal Union mabao 4-0.
Yanga: Juma Kaseja, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro', Kelvin Yondani, Frank Domayo ‘Chumvi', Simon Msuva, Hassan Dilunga, Didier Kavumbagu, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi.
Azam FC: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Said Moradi, David Mwantika, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy', John Bocco, Kipre Tchetche, Hamis Mcha ‘Viali'/ Kelvin Friday.
Mara baada ya mpira kumalizika, mashabiki wanaosadikiwa kuwa wa Azam, walijipanga nje ya uwanja na kulifuata basi la Azam huku wakiimba Sure Boy hatukutaki… Sure Boy hatukutaki… wakidai amekosa nafasi nyingi za kufunga.
Katika hali ya majonzi, shabiki mmoja aliyejulikana kwa jina la Deodatus Isaya ambaye ni Meneja wa Baa ya Rose Hill ya Segerea, alifariki dunia uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa Daktari, Nassoro Matuzya, shabiki huyo wa Yanga alianza kuishiwa nguvu mara baada ya Yanga kupata bao, ambako alishangilia kwa nguvu kabla ya hali hiyo kumkumba na kuchukuliwa na wahudumu wa Msalaba Mwekundu na kwenda kupewa huduma kwenye vyumba maalumu uwanjani hapo, lakini wakati akiendelea kupewa huduma ya kwanza alifariki dunia na mwili wake kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
Source: Tanzania Daima