Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,303
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amesema ujenzi wa barabara ya Mbinga -Mbambabay kiwango cha lami utafanyika kwa kipindi cha miezi 33 na kugharimu zaidi ya Sh129bilioni.
Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 67 tayari imeanza kujengwa, kubainisha kuwa mkandarasi ambaye ni kampuni ya Chico kutoka China ameshalipwa.
Akizungumza leo Jumatatu Januari 15, 2018 Kwandikwa amesema, “Ujenzi umeanza hatua za awali, mkandarasi ameanza kuchukua sampuli za udongo kwa ajili ya utafiti sambamba na kupeleka mitambo eneo la ujenzi.”
Mkazi wa Mbambabay, Emmanuel Mahena ameiomba Serikali kuwasaidia wazawa kupata ajira ndogo ndogo katika mradi huo kwa maelezo kuwa hatua hiyo itawapa unafuu wa maisha.
“Kazi tunazoweza kupewa ni kama za udereva na upishi,” amesema.
Mkazi wa Nyasa, Juma Tele ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi huo ili kurahisisha huduma za usafiri na kuchochea biashara.
Muungwana