SGR fanyieni kazi changamoto hizi

SGR fanyieni kazi changamoto hizi

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
5,168
Reaction score
8,981
Kwa sasa treni inasafiri kati ya Dar na Moro. Ni vizuri wahusika wakafanyia kazi baadhi ya mambo kabla usafiri haujatanuka kufikia maeneo mengine. Baadhi ya changamoto ni hizi hapa.

Kwenye stations maeneo ya kukaa abiria ni finyu hii inasababisha msongamano mkubwa ya watu.

Kwenye stations kuna viti vichache wakati kuna abiria wengi na wengine hawawezi kusimama muda mrefu kutokana na umri, magonjwa...

Kwenye stations hakuna usafiri wa uhakika na unaoeleweka wa kuchukua na kuleta abiria. Yani maajabu pale morogoro mkishuka hakuna hata kituo cha daladala. eti saivi ndio wameanza kujenga kwa spidi ya konokono!! Ina maana muda wote mradi unajengwa mamlaka zililala kuandaa maeneo haya kuweza kupokea watu.

Kwa sasa boda na bajaji ndio zinachukua watu kutoka hivi vituo. Yani hakuna maandalizi kabisa. na kwa kuwa hakuna bei elekezi kutoka maeneo haya hawa Boda na bajaji wamekuwa wanalipuka tu na bei zao toka kichwani. Hii inaleta usumbufu na mabishano yasiyo tija na kwa pale morogoro utaona idadi kubwa ya abiria wanaamua kutembea kuelekea barabara kuu.

Wengine wataongezea....
 
Waruhusu mizigo kwa kulipia kila uzani unaozidi kilo 30, kama wafanyavyo kwenye ndege. Ila waweke ukomo wa uzito wa mizigo yote isizidi kilo 60.
 
Wamejitahidi....ni mwanzo mwema.
Mwanzo upi? Kujenga reli ya mabilioni halafu usijenge miundombinu ya kupokea abiria? Kwa hiyo wakishuka walale hapo? Mbona Msamvu bus terminal imejengwa na parkings nzuri kabisa kwa ajili ya tax, bajaj etc??
 
Back
Top Bottom