Serukamba aibwaga tena CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serukamba aibwaga tena CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ALHAMISI, SEPTEMBA 06, 2012 | NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

  MAHAKAMA ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali ombi la kutaka mahakama hiyo ifanye mapitio katika hukumu iliyotolewa katika kesi ya uchaguzi kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, yaliyompa ushindi, Peter Serukamba (CCM).

  Uamuzi huo ulitolewa mjini hapa jana na jopo la majaji watatu Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Benard Luanda na Jaji Salum Masati waliokuwa wakisikiliza maombi hayo.

  Majaji wote watatu kwa pamoja jana walifikia uamuzi wa kutupilia mbali ombi hilo, lililowasilishwa na aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Mlei, kwa sababu ombi hilo limewasilishwa kimakosa.

  Katika uamuzi huo uliotolewa jana, majaji wameungana na Wakili wa Serukamba kwamba, Mlei alitakiwa kukata rufaa na si kuwasilisha ombi la mapitio ya rufaa.

  "Ingawa rufaa ni haki ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 38(4) ambayo inasomeka kutakuwa na haki ya kukata rufaa mbele ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya shauri lolote lililosikilizwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

  "Hivyo kwa sababu Mlei hakutimiza masharti hayo mahakama hiyo ikatupilia mbali maombi yake, hata hivyo Mlei anayo haki ya kukata rufaa," mwisho wa kunukuu.

  Machi 28, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, ilitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na Mlei kwa sababu alishindwa kuthibitisha tuhuma zake.

  Mwishoni mwa Agosti, mwaka huu, Mlei aliwasilisha maombi katika Mahakama ya Rufaa, akiiomba ipitie hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji Stella Mgasha.

  Akizungumzia hukumu hiyo nje ya mahakama, Serukamba, alisema imedhihirisha kwamba mahakamani si mahali pa kupeleka porojo zinazozungumzwa katika vijiwe vya wauza kahawa.

  "Ni kweli Mahakama imetupilia mbali mapitio ya hukumu ya uchaguzi wa Kigoma Mjini, sasa imedhihirisha kwamba, mahakamani si mahali pa kupeleka maneno ya vijiweni.

  "Kimsingi, wapiga kura wangu wamefurahi baada ya uamuzi uliotolewa leo (jana) na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania," alisema Serukamba.

   
 2. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  asante kwa taarifa
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Mawaki mawakili mawakili wa UPE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! This is a very basic procedure in courts of law, that whenever there is room for appeal, it can not be overriden by a review! Wakili gani huyo hajui, ndio hao anaowasema Lisu! hata mimi ambaye sio mjuzi wa sheria hilo kila mmoja analijua. Ni sawa na "Functus officio"- huwezo rudisha shauri hilo hilo lisikilizwe na mahakama hiyo hiyo kwa facts zile zile! hata sisi wa vijijini tunajua!
   
 4. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mwache ale kipindi chake cha mwisho, nakuambia iwe isiwe Serukamba hatapita tena Kigoma mjini yaani hata atengeneze mtandao wa namna gani,wanaKigoma kutokea Katonga, Kamara, Mwanga, Mji mwema, Majengo kote huko ndo kuna wapiga kura lakini walishamchoka zamani za mkoloni
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Usiusemee moyo wa mwenzio!
   
 6. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama gamba wanauwezo wajaribu 2015 hilo jimbo letu wanatucheleweshea tu
   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na bado haya majinga yataumbuka kwenye rufaa ya mvutabangi wao Lema
   
 8. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  mr ally inabidi amuachie jamaa amalizie
   
Loading...