Serikali Zimbabwe Yafunga Internet

Vikokoteo ni tatizo kubwa sana kwenye Bara letu. Hichi kikoteo kingine kimedai leo eti matatizo ya nchi yetu yasipopatiwa solutions kwenye awamu hii basi hayatapatiwa solutions milele!

Hata Baba wa Taifa hakuwahi kutoa kauli ya kujipaisha/kujikweza kiasi hiki.

Mwaka wa nne huu sijaona tatizo lolote lile nchini alilolipatia solution badala yake anaongeza matatizo. Mfano mmoja ni
Hatari sana Mkuu huyu Jamaa nisiendeleye kuongea! Ila usani wa kale sana!
 
Kufunga Internet itasaidiaje kuukwamua uchumi wa Zimbabwe? Akina Mnangagwa ni tamaa tu ya madaraka, otherwise, hawana lolote kazi kuiba kura tu.

Ukishakosana na watu wanaodhibiti uchumi wa dunia lazima ujiandae kukabiliana tu na haya na wala sio China au Russia awezaye kukusaidia make hata wenyewe wanapambana na vikwazo vyao.

Nashangaa kuna mtu alikuwa anasifia wachina eti wana misaada isiyo na masharti hajui kuwa hata Zimbabwe wako na mchina lkn hali ndio hiyo. Afrika hatuna jinsi lazima tufike mahali tukubali kuheshimu matakwa ya watu wetu. .

There is always no short cut to success and the luck is always against the one who depends on it. It's an open secret that ZANU PF is no longer the party of choice to most Zimbabweans and the same applies to the western powers. That's it.
 
Huu mtindo wa kuzima zima internet ni wakifala sana " naona unaibuka kwa kasi kubwa mnoo Africa ... naomba wananchi wa Africa tuamke na siku wa kithubutu kufanya hivi tuandamane " ili kuweza kuuondoa huo utawala madarakani ... haiwezekani uzime internet kwa sababu " hayo ni mawasiliano kama ambavyo yalivyo mawasiliano mengine " unapo funga internet ina maana kwamba kuna watu na makampuni kibao yanaingia hasara " kwa sababu yana tegemea kingiza mapato kwa kutumia internet " kwa mantiki hii uchumi wa nchi una simama " kwaajili ya ujinga wa interest za watu "..... matatizo ya wananchi hayawezi kutatuliwa kwa kuzima internet .... period

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali mpya inapitia kwenye njia zile zile za ile iliyopita tena hili ni jaribio baya zaidi la kujaribu kusilence watu wasitoe hisia zao....!!
Afrika inakabiliwa na tatizo la kimfumo na si kubadili watawala bali tubadili mifumo inayosimamia mamlaka za kiutawala kupitia katiba zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Zimbabwe hakuna serikali mpya serikali ni ile ile na mawazo ni yaleyale hakuna upya pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanasiasa na watu wa ajabu sana wakati wa kumtoa Mugabe eti jeshi likadai haliwezi wapiga raia wanaoandamana ili ionekane Mnangagwa ni nimtu wa watu thou ni jitu lile lile tu ambalo lilikuwa pamoja na Mugabe likaona anataka litosa ndo likaja na mapinduzi, sasa hivi wanaandamana kudai haki wanapigwa
 
Huu mtindo wa kuzima zima internet ni wakifala sana " naona unaibuka kwa kasi kubwa mnoo Africa ... naomba wananchi wa Africa tuamke na siku wa kithubutu kufanya hivi tuandamane " ili kuweza kuuondoa huo utawala madarakani ... haiwezekani uzime internet kwa sababu " hayo ni mawasiliano kama ambavyo yalivyo mawasiliano mengine " unapo funga internet ina maana kwamba kuna watu na makampuni kibao yanaingia hasara " kwa sababu yana tegemea kingiza mapato kwa kutumia internet " kwa mantiki hii uchumi wa nchi una simama " kwaajili ya ujinga wa interest za watu "..... matatizo ya wananchi hayawezi kutatuliwa kwa kuzima internet .... period...

Yaani ni Upuuzi usio na kichwa wala miguu. Ni kwamba Internet imekuwa kama basic need kwa dunia ya leo.
Uchumi wa nchi unapumulia mashine halafu hao hao Viongozi ndio wanaenda kuongeza matatizo mengine ya ku block, Communication and Connection kwa sababu ya Uoga.

Halafu Mnangagwa kaenda Davos kwenye World Economic Forums kutafuta 'WAWEKEZAJI' wakati ZiM inawaka moto.

Only in Africa!
 
Back
Top Bottom