My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,335
Nimeiona mkuuNadhani umeona like yangu huko
Intelligence ya Kenya ipo vizuri kuliko Tanzania, intelligence ya Kenya ipo busy kuinua uchumi wao wakati ya Tanzania bado inawaza kuua hata mtoto mchanga anayetoka familia ya Chadema.Kenya, Odinga ametangaza hakuna kukopa. Jamaa wanatuacha Kama tumesimama vile
Dunia ina nchi zaidi ya 200,(mataifa) na Kila nchi ina muundo wa serikali yake.
Zipo serikali mbaya na pia zipo serikali nzuri, na ktk serikali hizo nzuri na mbaya, ndani yake pia zipo serikali za Kijambazi.
Kuna aina mbili za ujambazi wa serikali.
1)Serikali inayopora mataifa mengine iwe kwa nguvu, kwa kurubuni, kwa kutapeli na kisha kilichoporwa huletwa nyumbani ili kufaidisha wananchi (Hizi ni serikali bora na nzuri )
2)Serikali inayopora haki za wananchi wake, kwa kuwabambikizia mzigo mkubwa wa kodi, kuwafumba midomo ili wasihoji mwenendo wa raslimali zao ,kuua Demokrasia inayojenga utawala bora, kujilimbikizia mali na kuishi maisha ya anasa.
Hizi ni serikali hatari sana za Kijambazi, mara nyingi huwa ni serikali za madikteta, zinakuwa zinaungwa mkono na kundi dogo la watu wanaofaidika nazo na mambumbumbu wengi wasio jua lolote, ambao wakishiba tu basi hawana la ziada hapa Duniani.
Ole wako ufungue mdomo hadharani kukosoa au kuhoji kasoro yoyote, jela au kaburi ndo itakuwa salamu yako.
Mataifa mengi ya Africa yana aina hizi za serikali za hovyo.
Wananchi ndo wanakuwa target ya kuporwa, unaamka asubuhi unakamatwa na kuambiwa wewe ni mhujumu uchumi, unafunguliwa kesi kisha hata kabla mahakama haijakukuta na hatia, unaambiwa uandike barua ya kukiri kuwa wewe ni mwizi wa nchi, yaani mhujumu uchumi, ukiri kuwa wewe ni mwizi halafu ukubali kurudisha ulichokiiba.
Vinginevyo utaendelea kusota mahabusu na kesi haina dhamana, na tayari una miaka mitatu jela na afya yako imedorora mno.
Aina ya serikali hizo hutumia nguvu kubwa mno kuzima sauti ya upinzani ili kukwepa kuumbuka juu ya maovu yake.
Unakuta ndani ya serikali hizo kuna kiongozi alikuwa anatumia sh mil 152 kwa siku eti kwa matibabu tu kwa muda wa miezi sita, kuna uhujumu uchumi unaozidi hapo?
Kuna matibabu gani ya mtu mmoja ya $ 125,0000 kwa siku hapa Duniani? iko wapi hiyo hospital inayotibu mtu mmoja kwa siku kwa hiyo gharama? iko nchi gani na inaitwaje?
Serikali za aina hiyo hupenda kusifiwa hata Kwenye hamna, ni Kama alivyokuwa Mobutu na Bokassa wa Central Africa.
Hizo ni serikali hatari na huwa haziondoki madarakani Kwenye sanduku la kura bali Kwenye sanduku la moto.
Jambazi linajitetea...jf kweli imejaa demokrasiWewe mtoa Mada, sijakuelewa. Yani mafisadi waache kushughulikiwa kisa utawala bora??? Wahujumu uchumi wengi wamejificha chini ya demokrasia na utawala bora.
Nikihakikishie jambo moja, Nchi nyingi za Africa bado hajikomaa kufikia hatua ya kuwa na demokrasia na utawala bora. Mfumo wa ni imra ndio haswa unatakiwa kwa nchi za Afrika ili kujenga nidhamu na kuleta maendeleo kwa nchi na wananchi kwa ujumla.
Angalia nchi kama Libya, Egypt, Iraq, Syria na mataifa mengine yalipata maendeleo na kustawi chini ya utawala wa ki imra na hali ilivyo sasa.
Mataifa ya magharibi yametuletea demokrasia yakijua fika afrika bado haijakomaa kiasi cha kutosha kwenda na mfumo wa kiutawala wa kidemokrasia kwasababu ya low level of civilization, literacy, etc.
Hata mataifa ya magharibi unayoshabikia yana serikali bora ili yametoka kwny mfumo wa ki imra kabla ya kujikita kwny demokrasia.
Acha ushabiki wa kisiasa na mambo yasiyokuwa na msingi kwa nchi za kiafrika.
Umeleta Mada ya kipumbavu kabisa.
Wewe mtoa Mada, sijakuelewa. Yani mafisadi waache kushughulikiwa kisa utawala bora??? Wahujumu uchumi wengi wamejificha chini ya demokrasia na utawala bora.