Serikali yoyote duniani ni yenye kujali watu wake ccm imefanya mema gani awamu hii

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Tangu serikali hii iingie madarakani tumrshuhudia ubabe usiotumia akili na busara alianza kwa tumbua tumbua lakini mwisho akaishia kula matapishi yake. Failure ikajionyesha wazi.

Pili likaja la watumishi hewa akawapata wengi sana ninakumbuka walifika elfu kumi na moja lakini cha ajabu bajeti ya mishahara ikapanda badala ya kushuka. maswali yalikosa majibu. Tena tatizo likajionyesha operation ikaleta dosari na hasara kuliko faida. Failure ikajionyesha wazi tena.

Tatu vyeti feki nayo ilikuwa operation mojawapo ya utumishi wa umma ili kuleta nidhamu na ufanisi ktk utumishi wa umma. zoezi hili lilienda mpaka ilipifika kwenye wakubwa walioanzisha wakaona waanze kushambulia watu kisa wameambiwa na wao mbona nao wana feki ishu ikawa ngumu kumeza. Hivi sasa swala hilo ni kama halipo vile maana imekuwa ngumu kukamata watu. Harufu ya kufeli naiona mbeleni siombei itokee.

Nne operation mbili hapo juu zilitibua utaratibu ktk utumishi wa umma kila kitu kilisimama kupandisha vyeo, kuongeza ongezeko la kila mwaka wa fedha, uhamisho, malipo ya madeni, ajira ya watumishi wapya na kusababisha msongo kwa baadhi ya watumishi.

Sasa huu ni mwaka wa pili mkuu anaonekana hana mpango kuendelea na utaratibu wa kawaida. Watu wanajiuliza
serikali kazi yake nini hasa kama haiajiri, haiwapi watumishi wake stahiki zao, wakati wa majanga haitoi msaada kazi ya serikali ni nin hasa?

Je kweli kuna kazi kubwa kama kujenga uchumi wa nchi yako kwa kuwapa moyo watu wanaovuja jasho lao kwa ajili ya taifa? Kama serikali haioni hilo nani afanye hilo?

Njaa inawapiga watu bado mku na serikali yake wanatoa vitisho eti hakuna njaa kazi ya serikali nini basi?

Wananchi tukatwe kodi zetu kwa ajili ya nini kama vitu vyote nilivyovitaja hapo juu serikali imegoma kuteleza kwa visingizio kibao.

Tunawezaje kuwa wazalendo kwa nmna hii mbaya ya kukatisha tamaa watu. Mzazi aliyemsomesha mtoto wake mpaka chuo kikuu hajaajiriwa mpaka leo huu mwaka tatu kama sio msiba nyumbani ni nin kwa mzazi?

Lazima mkuu ajue ametukosea sana watanzania. Nchi hii imefikia hapa kwa uzembe wa rafiki zake waluotangulia. Asiwe na hasira na watanzania wssio na hati Wakati wenye umewaacha wanakula kwa mrija.

Asifurahie kuturundikia kodi akumbuke kurudisha kwetu kwa kwa kutoa ajira kwa watanzania na kuwashughulikia mafisadi bila kinyongo na makundi mbalimbali ktk jamii.

karibuni wanajavi tujsdili mustakabali wa nchi yetu.
 
Wanajitahidi kuleta maendeleo ya Vitu kama Ndege,Reli,Viwanja vya Ndege na Barabara.Baadae watakuja kwenye Maendeleo ya Watu kama Mishahara minono,Huduma Bora za Afya,Elimu bora na Chakula.
 
Wanajitahidi kuleta maendeleo ya Vitu kama Ndege,Reli,Viwanja vya Ndege na Barabara.Baadae watakuja kwenye Maendeleo ya Watu kama Mishahara minono,Huduma Bora za Afya,Elimu bora na Chakula.
Hizo ndege anapanda nani na uchumi huu? Hapo mwanza hakuna tena ndege kubwa za jet zinazokwenda maana zilikuwa zinaenda viti vitupu....zimebaki panga boi.
 
wameanzisha vita ya madawa ya kulevya kwa kuwasaidia watuhumiwa kufanya biashara hiyo haram kwa umakini zaidi ili kizazi kijacho kiwe na mataahira wengi zaidi na ccm itawale milele
 
nadhani ni vzr watu tuelewane hakuna jambo la maana alilofanya
 
Uchumi unakuaje,mnakataza pombe za viroba,wafanyabiashara wa ndan mnawasumbua,mfano manji,mmevunja nyumba za watu,et wanakaa mabonden.nk
 
Back
Top Bottom