Serikali yetu vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yetu vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tambarare, May 30, 2011.

 1. t

  tambarare Senior Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amesema wakazi wa vijiji kadhaa vya wilaya ya Mbarali ambavyo vimo ndani ya ramani ya hifadhi ya bonde oevu la Ihefu kuwa wanapaswa kuondoka ili kulinda hifadhi ya bonde hilo.
  Maige alihitimisha kauli ya serikali mjini Rujewa juzi baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo ikielezea hali ya mgogoro wa muda mrefu uliosababisha baadhi ya wananchi waendelee kuishi ndani ya hifadhi hiyo na vijiji vingine vitano kufungua kesi kwenye mahakama ya ardhi kupinga kuondolewa katika maeneo yao.
  Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri Maige amechoshwa na taarifa zinazoelezea mgogoro wa kuwaondoa wananchi katika bonde la Ihefu kwa kiasi kikubwa alionyesha wazi kutokukubaliana na ushawishi wa mbunge wa jimbo hilo, Modestus Kilufi, aliyeonyesha wazi kuwaunga mkono wananchi waliogoma, ili waendelee kuwepo kwenye vijiji hivyo.
  Alisema suala la Ihefu sio la kijimbo wala wilaya isipokuwa ni la kitaifa na kwamba uchumi wote wa nchi katika uzalishaji mali unategemea hifadhi hiyo ambayo ndiyo chanzo kikuu cha maji yanayoingia kwenye mto Ruaha Mkuu na kupeleka maji Mtera na Kidatu kwa ajili ya kuzalisha umeme.
  “Mheshimiwa mbunge mwenzangu umeona wenzetu wanavyoandamana wakiwaeleza wananchi tatizo la umeme. Sisi tunataka kupingana na msimamo wa serikali yetu, tutakuwa kwenye hatihati wakati wa uchaguzi mkuu ujao, ukishinda pekee yako na majimbo mengine tukapoteza utaunda serikali?” alihoji huku akionyesha kutoridhishwa na kundi la wananchi wachache wasiopenda kuondoka hifadhini.
  Awali, mbunge wa jimbo hilo, Kilufi alisema mwisho wa mgogoro huo unahitaji maridhiano kati ya serikali na wananchi na endapo maridhiano hayo hayatafikiwa itakuwa vigumu zoezi hilo kutekelezwa.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi alipinga kauli zinazotolewa na wadau mbalimbali kuwa shirika hilo halitosheki na maeneo linayopewa na kujipanulia kinyemela mipaka na kusema dhana hiyo ni potofu kwani TANAPA inasimamia maeneo hayo kwa niaba ya serikali na hawahusiki na upimaji wa mipaka.
  NASHINDWA KUIELEWA HII SERIKALI KWANI MAENEO HAYA YA MBARALI MASHAMBA YA NAFCO WAMEMUUZIA MUWEKEZAJI(WEZI WA NCHI YETU) SASA WANAINCHI WANAHANGAIKA MAENEO YA KILIMO,,,,,SASA HIVI WANAAMBIWA WAHAME HIVI KAMA WANAINCHI WALIVYO BID TENDA YA KULIENDESHA SHAMBA NA WAKAPEWA KUNGEKUWA NA MATATIZO YA KILIMO???????? HAYA MUWEKEZAJI MWENYEWE(WEZI WA NCHI YETU) ANAPANDA MIBONO BADALA YA MPUNGA...........KWELI KIKWETE HATUTA KUSAHAU KAMWE MUNGU AKUPE UHAI MREFU ILI VIZAZI VYETU VITAKAPOKUJA ANDIKA HISTORIA MPYA
  SOURCE...TANZANIA DAIMA
   
Loading...