Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Wakati Serikali yetu kipenzi ikiwa kwenye pilika pilika za kuhamia Dodoma Mji Mkuu wetu, nashauri jambo moja ambalo tunapaswa kujifunza kutokana na Historia yetu!
Serikali isikubali kurudia makosa yaliyofanywa Dar na Miji mingine nchini mwetu, Miji ambayo ilijengwa kwa misingi ya Ubaguzi au apartheid dhidi ya sisi wenyeji, Watanzania weusi!
Kwa wasio fahamu Mji wetu wa Dar kama tuujuavyo leo hii ulipangwa na kujengwa kwa sehemu kubwa sana na Wakoloni Wajerumani na hapa naongelea Dar ya zamani maeneo kama Oysterbay, Msasani, Upanga, Kinondoni, Magomeni, Kariakoo, na sehemu kubwa ya Wilaya ya Temeke na Ilala ya leo!
Wajerumani walitumia mfumo wa Kibaguzi au apartheid kuupanga Mji wa Dar ambao walitenga maeneo ya Wazungu, Waarabu na Wahindi na mwisho maeneo ya Waswahili na ndiyo maana mpaka leo hii tunatumia misemo kama Uswahilini tukimaanisha tunapoishi Waswahili, Uhindini wanapoishi Wahindi na Uzunguni waishipo Wazungu na ubaguzi huu tumeurithi, kuukubali na kuusambaza Mikoani kote mpaka leo hii kila uendapo kuna maeneo ya Uzunguni au Uhindini na Uswahilini ambapo unaweza kupaita Ubayani!
Cha ajabu labda kuliko vyote nchi yetu ilikuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa kibaguzi ujulikanao kama apartheid huko nchini AK wakati hapa nyumbani kwetu apartheid ipo na tunaiishi kila siku!
Sasa kwa kuwa tumepata bahati ya kujenga Mji wetu wenyewe basi tuondoe kabisa hii Misamiati ya Uzunguni, Uhindini na Uswahilini kwani bila ya kufanya hivyo tunakuibali apartheid dhidi ya watu wetu wenyewe bila ya sisi kujua!