Serikali Yetu Inajali Afya za Wananchi Wake?

Serikali Yetu Inajali Afya za Wananchi Wake?

Asamwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
3,802
Reaction score
2,570
Wadau wote wa JF heshima kwenu.

Kuna wakati najaribu kufikiria sana matatizo mbali mbali yanayotukabili sisi wananchi wa Tanzania na hatua ambazo serikali yetu inachukua ili kuyapatia ufumbuzi. Kwa kweli inasikitisha!

Kwa kifupi, naweza kusema kuwa Serikali haichukui hatua zo zote za dhati katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo yanawakabili wananchi wake. Kwa leo, nitazungumzia swala la mboga mboga kama kabeji, nyanya, matango, karoti nk.

Wananchi wengi wameacha au wamepunguza sana kula mboga mboga zinazouzwa katika masoko yetu kutokana na ukweli kuwa si salama kwa afya. Hii ni kwa sababu wakulima huzipiga dawa za wadudu zisizostahili (sumu) au hupiga dawa zinazostahili muda mfupi sana kabla ya kuvuna.

Hili swala limeshalalamikiwa na watu wengi sana, lakini sidhani kama kuna hatua zo zote za maana ambazo zimewahi kuchukuliwa na Serikali ili kulikomesha.

Sina hakika pia kama mabwana afya wanafanya ukaguzi wa mboga mboga kwenye masoko yetu ili kuhakikisha kama ziko salama kwa matumizi ya Binadamu. Wangekuwa wanafanya ukaguzi tungekuwa tumeshapata taarifa kuhusu uteketezaji wa mboga mboga ambazo si salama, pamoja na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika.

Je, ni vigumu Mabwana Afya kufanyia uchunguzi sampuli za mboga mboga, na kuteketeza zile ambazo si salama kwa matumizi ya binadamu pamoja na kufuatilia wahusika na kuwachukulia hatua kali?

Je, kuna jitihada zo zote ambazo zinafanywa kuwaelimisha wakulima wa mboga mboga kuhusu madhara ya kutumia dawa ambazo si sahihi?

Kwa kweli kama Serikali kupitia Wizara husika haitaliangalia kwa makini hili swala, wananchi wataendelea kupata athari za kiafya ambazo chanzo chake ni mboga mboga zilizolimwa kinyume na taratibu zinazokubalika.

Wadau nawasilisha.
 
Mkuu mtanzania linda afya mwenyewe, hii serikali ukiitegemea utajikuta unapoteza maisha, mabwana afya wenyewe wamebakiza kulewa tangu asubuhi na kuvizia rushwa toka kwa mama ntilie..!!!
 
Baba V nimekupata; ila kama itabidi kila mtu alinde afya yake mwenyewe majukumu ya Serikali ni yapi?
 
Mkuu hili ni million $ question! Kama inajali afya zetu, wao wasinge enda nje kutibiwa, wasingewafungia madaktari zaidi ya 300 kwa zaidi ya mwaka, wasinge leta Bajaj ambulance wakati wao wanatembelea mashangingi and more you can help to name
 
Back
Top Bottom