Rashford Lingard
JF-Expert Member
- Feb 9, 2018
- 938
- 1,152
SIKU chache baada ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kusajili na kuthibitisha dawa tano za asili ikiwemo Ujana inayotibu nguvu za kiume, imebainika kuwa suala hilo limezua balaa la aina yake mitaani kwa wanandoa kuvutana kwa ajili ya kuzisaka dawa hizo huku pia baadhi ya watu waliokuwa wakiuza dawa za tatizo hilo wakilalamikia kukimbiwa na wateja.
UCHUNGUZI WA UWAZI
Uwazi liliingia mtaani kufanya uchunguzi wa mapokeo ya watu wa kada mbalimbali ambao walitoa maoni yao kuhusu ‘neema’ ya ujio wa dawa hiyo katika jamii na kubaini jinsi ilivyozua balaa katika familia mbalimbali.
Katika maeneo ambayo Uwazi lilifika jijini Dar, ilibainika kwamba, wanandoa wengi wapo kwenye mshikemshike nguo kuchanika wakivutana katika kutafuta suluhu ya tiba kwani tatizo hilo limekuwa likiwatesa kwa muda mrefu.
“Mimi nilioana na mke wangu miaka kumi iliyopita, lakini kimsingi sikuwahi kuifurahia ndoa yangu. Tumevutana sana na mke wangu. Kuna wakati ilifikia mahali hadi akaamua kuondoka nyumbani. Baadaye tulifanya mazungumzo na wazazi, akarudi.
VUMBI LA KONGO
Kwa upande wao wauzaji wa Vumbi la Kongo, walisema kuwa, nao wameathirika na kauli ya serikali kuzithibitisha dawa tano za asili ikiwemo Ujana kwani wa¬likuwa wakifanya sana biashara kabla.
TUMEFIKAJE HAPA?
Machi 13, mwaka huu, Msajili wa Baraza la Tiba za Asili na Mbadala, Dk Ruth Suza, katika mkutano na waandishi wa habari, alitan¬gaza kuzithibitisha dawa tano za asili ikiwemo hiyo ya Ujana inayotibu nguvu za kiume.
Mbali na Ujana, dawa nyingine alizozitaja ni IH Moon, Coloidal Silver, Sudhi na Vatari zinazotibu magonjwa mbalimbali.
Pia Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alizitaja dawa nyingine mbili za aina ya Sildenafil na Tadalafil zinazotoka nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia tatizo hilo la nguvu za kiume.
Awali, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile (pichani uk. 3) katika mkutano huo, alimuagiza katibu mkuu wa wizara yake, Dk Mpoki Ulisubisya kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti wa afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu na pia kujua ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kwa kiasi gani nchini.
Waziri huyo alitoa agizo kwa waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala kuacha mara moja kutoa matangazo yao mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mabango ya barabarani kuhusu tiba ya ugonjwa huo.
“Tumeendelea kuishi hivyo na mimi nikawa ninajaribu kutumia dawa mbalimbali za asili bila mafanikio. “Utaambiwa mara sijui kuna dawa hii, mara utaambiwa kuna dawa ile, lakini zote hazikunipa matokeo mazuri,” alisema mkazi mmoja wa Bunguruni jijini Dar huku akiomba hifadhi ya jina.
BAADA YA SERIKALI KUTHIBITISHA
Mkazi huyo wa Buguruni alizidi kueleza kuwa, mara baada ya serikali kutangaza kuzisajili na kuzithibitisha dawa hizo tano za asili, mkewe amechachamaa upya na kumtaka ahakikishe anazitafuta na kuzipata ili angalau naye afurahie tendo la ndoa.
“Yaani huwezi kuamini, badala ya kuwa furaha, imekuwa tena ugomvi. Nimemwambia ninajaribu kufuatilia kwa makini ili ninunue maana kimsingi serikali yenyewe imetangaza tu kuzisajili, lakini haikusema zinapatikana wapi.
“Sasa wakati mimi nikiwa ninatafuta suluhu, yeye (mkewe) anaona kama vile labda silitilii maanani. Sasa ukirudi tu nyumbani kabla hamjaongea lolote ishu kwanza ni hizo dawa,” alisema mwananchi huyo.