Serikali yazitaka TRA na TPA kubaini chanzo cha kupungua kwa shehena za kontena bandarini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.

Hata hivyo, Dokta Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

"lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam
 
Sababu zinajulikana, gharama za usafirishaji mizigo kwenda hizo nchi ziko juu sana kwa vile hatuna reli. Ujinga aliotutia Kikwete wa kuegemea kwenye malori na kuua reli yetu leo unatugharimu. Kusafirisha mizigo kwa malori ni gharama kubwa sana, na pia ufanisi zero ukijumlisha na uharibifu wa barabara.
Kwa ujinga huo huo JK akataka tuanze kujenga bandari nyingine kwao Bagamoyo kabla hatujapata suluhisho la kusafirisha kwa gharama nafuu mizigo ya bandari ya Dar. Upuuzi mtupu.

Dr Mpango na Dr Magufuli, msitafute mchawi, suluhisho ni STANDARD GAUGE RAILWAY
 
Tatizo ni vilaza na wajinga waliojaa kwenye taasisi nyeti na kushindwa kulisaidia taifa, uwezo wa waajiriwa wengi kwenye taasisi nyeti za taifa hili ni mdogo kwa dunia ya sasa ya ushindani, uwezo huu mdogo unasababisha ubunifu kukosekana na taifa kupoteza mapato mengi kijinga kabisa... Watu hawa wengi ambao uwezo wao kiakili ni mdogo na wapo kwenye taasisi nyeti limesababishwa na udini, ukabila,undugu na ubinafsi uliokithiri kwa kuweka maslahi binafsi mbele na si ya taifa..
 
Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina kwenye hili na haya mambo vinginevyo tutacheza mchezo wa paka na panya na tutarudi kule kule kwenye wizi na ufisadi, SYSTEM NA SEHEMU NYETI ZA TAIFA HILI LIMEJAZA VILAZA NA WAJINGA WASIOWEZA KUFIKILI KWA MANUFAA YA TAIFA HILI KWA MIAKA 100. KUNA HAJA YA KUANGALIA MFUMO MZIMA WA AJILA ZA TAASISI NYETI NA MFUMO MZIMA WA ELIMU KUANDAA KIZAZI CHA USONI, vinginevyo tunapoteza muda, HATUNA WATU WA KUTOSHA KWENYE TAASISI WALIO SERIOUS NA COMPETET KWENYE KAZI WANAZOZIFANYA..HILI NDIO TATIZO KUBWA KABISA LA MSINGI..
 
Tatizo ni vilaza na wajinga waliojaa kwenye taasisi nyeti na kushindwa kulisaidia taifa, uwezo wa waajiriwa wengi kwenye taasisi nyeti za taifa hili ni mdogo kwa dunia ya sasa ya ushindani, uwezo huu mdogo unasababisha ubunifu kukosekana na taifa kupoteza mapato mengi kijinga kabisa... Watu hawa wengi ambao uwezo wao kiakili ni mdogo na wapo kwenye taasisi nyeti limesababishwa na udini, ukabila,undugu na ubinafsi uliokithiri kwa kuweka maslahi binafsi mbele na si ya taifa..
Vilaza, mbumbumbu zote ndiyo ziko kwenye taasisi nyeti za serikali.
Imewekwa hapo na vilaza wenzao waliopo huko ngazi za juu hakuna wanachojua zaidi ya kutafuta tu.
 
Sababu zinajulikana, gharama za usafirishaji mizigo kwenda hizo nchi ziko juu sana kwa vile hatuna reli. Ujinga aliotutia Kikwete wa kuegemea kwenye malori na kuua reli yetu leo unatugharimu. Kusafirisha mizigo kwa malori ni gharama kubwa sana, na pia ufanisi zero ukijumlisha na uharibifu wa barabara.
Kwa ujinga huo huo JK akataka tuanze kujenga bandari nyingine kwao Bagamoyo kabla hatujapata suluhisho la kusafirisha kwa gharama nafuu mizigo ya bandari ya Dar. Upuuzi mtupu.

Dr Mpango na Dr Magufuli, msitafute mchawi, suluhisho ni STANDARD GAUGE RAILWAY
Asante sana kiongozi.
Ajuza akisoma hapo atarusha povu la kutosha
 
kinachotakiwa ni kuwa na timu ya watu kama sita ivi kwa ajli ya kwenda katika Nchi kama Zambia..Congo dr na Zimbabwe kuwaona wale ambao walikua wanapitisha mizigo katika bandari yetu na wameacha kama kuna kampuni moja ya Zambia ilipitisha Gari 500 kwa kutumia bandari yetu miaka miwili iliyopita kuna matatizi mengi walipata hapa kutoka kwa maagent wetu mpaka kupelekea kuhama na kuanza kutumia durban wafatwe wale na hao Tra sio msaada kabisa zaidi zaidi ni kupiga mnada mali za wateja...wafatwe hao wateja huko bandari ni biashara kama biashara zingine..
 
Hili suala la kupungua makontena lilijadiliwa hapa wiki imepita sasa. Lakini upinzani ulikuwa mkali washangiliaji wakasema ni taarifa ya uongo. Haya leo Mkulu mwenyewe kakili hilo, ila amenichanganya aliposema haijaathiri makusanyo ya nchi ilhali ukijumlisha hapo unaona kuna upungufu kama contena 1000 hivi je hayo yalikuwa yanapitishwa bure? Na kama yanalipiwa je hiyo hela ilikuwa inaenda wapi kama sio serikalini haiongezi kwenye makusanyo?
 
Sababu zinajulikana, gharama za usafirishaji mizigo kwenda hizo nchi ziko juu sana kwa vile hatuna reli. Ujinga aliotutia Kikwete wa kuegemea kwenye malori na kuua reli yetu leo unatugharimu. Kusafirisha mizigo kwa malori ni gharama kubwa sana, na pia ufanisi zero ukijumlisha na uharibifu wa barabara.
Kwa ujinga huo huo JK akataka tuanze kujenga bandari nyingine kwao Bagamoyo kabla hatujapata suluhisho la kusafirisha kwa gharama nafuu mizigo ya bandari ya Dar. Upuuzi mtupu.

Dr Mpango na Dr Magufuli, msitafute mchawi, suluhisho ni STANDARD GAUGE RAILWAY
Kikwete Kikwete Kikwete,get over it already.
 
Naona watu mnalizunguka buyu hamtaki sema ukweli.!!!
Tatizo Ni mizigo ambayo zamani ilikuwa ikisemekana Ni ya kwenda nje ya nchi lakini mwishowe zinaishia soko la ndani, sasa kwa sababu TRA wamebanwa hilo haliwezekani tena ndio maana inaonekana mizigo ya kwenda nje imepungua kitu ambacho sio kweli kwani waliokuwa wakiingiza hiyo mizigo Ni hao hao wa ndani
 
Containers nyingi zilizosemekana zilikuwa zinaenda nchi jirani. kiuhalisia zilikuwa zikiishia hapahapa Tanzania kwa minajili ya kukwepa ushuru!

njia za ukwepaji kulipa ushuru nyingi zimedhibitiwa, ile janja ya kusema zinaenda nchi jirani imepotea! Hata wanao agiza hapa nchini, hakuna namna ya kukwepa ushuru, hivyo ni jambo ambalo halikuzoeleka kwa wafanya biashara hasa wakubwa!

Ni mstuko tu wa upepo, utapita na wafanya biashara nchini mwishowe watazoea kulipa ushuru halilali!
 
Tatizo ni vilaza na wajinga waliojaa kwenye taasisi nyeti na kushindwa kulisaidia taifa, uwezo wa waajiriwa wengi kwenye taasisi nyeti za taifa hili ni mdogo kwa dunia ya sasa ya ushindani, uwezo huu mdogo unasababisha ubunifu kukosekana na taifa kupoteza mapato mengi kijinga kabisa... Watu hawa wengi ambao uwezo wao kiakili ni mdogo na wapo kwenye taasisi nyeti limesababishwa na udini, ukabila,undugu na ubinafsi uliokithiri kwa kuweka maslahi binafsi mbele na si ya taifa..
umesweep tu, taja nani ni nani tuelewe, unatuongeza mashaka tu!
 
Serikali imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.

Hata hivyo, Dokta Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

"lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam
 
watu walikua wanaongea humu jf kuwa mizigo bandarin imepungua but wakawa wanatukanwa kwamba ni waongo hawaipendi serikali
 
Back
Top Bottom