Serikali yaweka Vipaumbele 8 vya afya 2019/20

Serikali yaweka Vipaumbele 8 vya afya 2019/20

Joined
Sep 5, 2017
Posts
24
Reaction score
20
Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha mwaka cha wadau wa sekta ya afya kujadili vipaumbele vya utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

"Na hivi vipaumbele ndivyo ambavyo tutavifanyia kazi kama kuna mtu yeyote anataka kuja kufanya kazi na serikali basi vipaumbele vyetu katika sekta ya afya ni hivi na siyo vinginevyo,” alisema Waziri Mwalimu.

Alisema kuwa moja ya vipaumbele hivyo ni pamoja na kuimarisha huduma za afya ya uzazi ya mama na mtoto, lengo likiwa ni kupunguza vifo vya wajawazito.

"Kwa hiyo tumekubaliana tutaendelea kuweka miundombinu kwa ajili ya huduma za dharura na miundombinu kwa ajili ya watoto wachanga kwa sababu sasa hivi watoto wachanga takribani 9,000 wanafariki ndani ya siku 28," alisema.

"Lakini tumekubaliana kuongeza huduma za uzazi wa mpango kwa sababu imelezwa na wataalamu kuwa tunaweza kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 40 kama tutakuwa na njia za uzazi wa mpango zilizo salama na hapa hatukatazi watu kuzaa bali kuweka nafasi kati ya mtoto mmoja na mwingine mtoto," alisema Mwalimu.

Aliongeza kuwa katika eneo jingine walilokubaliana kulifanyia kazi ni eneo la afya za wasichana balehe pamoja na wavulana, kwa kuwa hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wasichana 10,027 wanapata ujauzito kabla ya kutimiza miaka 18.

"Eneo jingine ni kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto," alisema.

Katika eneo jingine Waziri huyo alisema kuwa ni kuendelea kuajiri watumishi katika sekta hiyo pamoja na kuimarisha huduma za afya.

Aidha, alisema wamekubaliana kuongeza raslimali fedha ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za afya katika maeneo mbalimbali nchini.

"Eneo jingine ambalo tumeliweka kuwa moja ya vipaumbele ni kuhakisha kuwa tunaimarisha upatikanaji wa dawa ikiwa ni pamoja na kufika kwa wakati na kutumika kwa usahihi na dawa muhimu kupatikana katika vituo vya afya kwa asilimia 90," alisema.
 
Kwanini anasisitiza hawawakatazi watu kuzaa, nani aliyewakataza in the first place?
 
Back
Top Bottom