VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Katika kile kinachoonekana kama kusaka kura kwa chama tawala-CCM,Serikali imeongeza mshahara wa watumishi wa umma kimyakimya. Kuongezwa kwa mishahara ya watumishi wa umma katika kipindi hiki,kunaonekana wazi kama kampeni.
Nyaraka za kimshahara toka Idara,Taasisi na Mashirika mbalimbali ya umma,zinaonesha kuwa mishahara imepanda kwa ongezeko la shilingi laki moja hadi laki nne kwenye mshahara wa mwezi uliopita. Ni wazi kuwa huku ni kuwarubuni watumishi.
Watumishi wa umma,kwa miaka nenda-rudi,wamekuwa wakilalamikia mishahara duni. Wapo walimu wanaoidai Serikali mabilioni ya shilingi. Wapo hata Wastaafu wa Jumuiya ya zamani ya Afrika Mashariki ambao nao wanasotea haki zao.
Siasa za kurubuni,kulaghai na kupumbaza tusizipe nafasi. Kwanini sasa ndiyo Serikaliwiwajali watumishi wa umma?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam