Serikali yatoa kanuni za Mifuko ya Jamii iliyounganishwa

Serikali yatoa kanuni za Mifuko ya Jamii iliyounganishwa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,730
Reaction score
62,942
Dar es Salaam. Baada ya kuunganisha mifuko minne ya hifadhi ya jamii Serikali imetoa kanuni mpya zinazozuia fao la kukosa ajira.

Kwa mwanachama atakayeachishwa kazi, kanuni zinasema atalipwa fao la kutokuwa na ajira ambalo ni sawa na theluthi moja (asilimia 33.3) ya mshahara aliokuwa anapokea akiwa kazini.

Kuhusu malipo hayo kanuni hizo zinasema, “yatadumu hadi miezi sita ndani ya mwaka mmoja mpaka mwanachama huyo atakapopata ajira nyingine. Endapo hatopata ajira mpya, mwanachama hatolipwa kwa zaidi ya miezi 18 kwa muda wote wa utekelezaji wa taaluma yake.”

Baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kuiunganisha mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF na kuunda mmoja kwa ajili ya watumishi wa umma ambao umeanza kufanyakazi kuanzia Agosti Mosi, 2018 kanuni mpya zimepitishwa.

Kabla ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo, kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu fao la kujitoa ambao hata hivyo, Serikali ilishikilia msimamo wa kuliondoa.

Agosti 17, Waziri Jenista Mhagama mwenye dhamana ya kazi na ajira nchini amesaini kanuni za Sheria ya Hifadhi ya Jamii kuruhusu kuanza kutumika kwake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Suimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii, Irene Kisaka alithibitisha: “Ni zenyewe. Zimepitishwa na zitaanza kutumika.”

Ikitokea mwanachama huyo hajapata ajira nyingine miezi 18 baada ya kupokea malipo ya kutokuwa na ajira basi atatakiwa kubadili michango yake kwenda mpango wowote wa kuchangia kwa hiyari aupendao.

Kiwango kitakachohamishwa kwenda mpango huo kitakuwa jumla ya michango yote kutoa pensheni aliyolipwa kipindi cha kukosa ajira. Mwanachama huyo ataendelea kuchangia mpango aliouchagua kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazousimamia.

Utaratibu wa fao la kukosa ajira linawahusu wale wanaofanyakazi za muda mfupi au za mkataba pia. Kwa mwanachama ambaye michango yake ni chini ya miezi 18 ambayo ni sawa na mwaka mmoja na nusu kanuni zinasema anastahili malipo ya pamoja kiasi cha asilimia 50 baada ya kuachishwa kazi.

Endapo ataendelea kukosa ajira kwa miezi 18 baada ya kupokea asilimia 50 ya michango yake, atatakiwa kujiunga na mpango wowote wa kuchangia kwa hiyari atakaoupenda.

“Kiasi kitachopelekwa kwenye mchango wa hiyari kitakuwa kilichobaki baada ya malipo ya awali, asilimia 50,” zinabainisha kanuni hizo.

Kama ilivyokuwa awali, kanuni zinasema mwanachama atastahili pensheni endapo atakuwa amechangia kwa kipindi kisichopungua miezi 180 au miaka 15.

Na yule atakayekuwa amechangia kwa kipindi hicho au zaidi lakini akaachishwa kazi kwa manufaa ya umma kabla ya kufikisha umri wa kustaafu, atalipwa kiinua mgongo lakini ataanza kupokea pensheni ya kila mwezi atakapofikisha umri unaokubalika.

Kanuni hizo zinatambua miaka 55 kuwa ndio umri wa kustaafu kwa hiyari na 60 kwa mujibu wa sheria.

Na mwanachama atakayeachishwa kazi kabla ya kufikisha umri wa kustaafu lakini amechangia chini ya miaka 15 au miezi 180, atalipwa kiinua mgongo pekee.

Uteuzi

Mwanachana ambaye amechangia kwa zaidi ya miezi 180 lakini hajafikisha umri wa kustaafu ila ameteuliwa kushika wadhifa wa kisiasa ambako kuna utaratibu maalumu kwa ajili yao, basi atalipwa kiinua mgongo wakati akisubiri kupokea pensheni atakapofikisha miaka 55.

Licha ya watakaoteuliwa, ikitokea mwanachama ameapunguzwa kazi, ofisi aliyokuwa anahudumu imefutwa au imefanyiwa marekesho hiyo nafasi yake imeondolewa lakini amechangia kwa muda huo, naye atakuwa na haki ya kupata kiinua mgongo na kusubiri pensheni atakapofikisha umri unaokubalika.

Chanzo: Mwananchi
 
Mambo mengi ya serikali ni kichefu chefu.

Unampangia mtu siku ya kuchukua pesa yake?
 
!
!
Dawa Yao Ndogo Tu Hawa Jamaa. Kujiajiri Tu Katika Mfumo Usio Rasmi Baasi. Unajisajili Kama Sole Proprietor, Unafanya Mipango Yako Baasi. Hakuna Cha Loan Board Wala Cha PAYe Wala Sijui Makato Gani.
 
Dah, yaani pesa yangu ajira sina nataka nitoe pesa YANGU ila bado mazinguliwa. Hii nchi hatari sana. Sioni point ya kumsaidia mwananchi wa chini hapa.
 
Wabadili sheria,umri wa kustaafu kwa hiari uwe 50,badala ya 55.
Vijana waliosoma taaluma mbalimbali nao wajipatie ajira,maisha yasonge.
 
Hio mifuko ingefanywa iwe hiari kujiunga ingependeza kuliko kulazimishwa
 
jamii forum
Ndo nimeamini siasa za kiAfrika ni siasa uchwara,yaani hapo ni kama wameamua kuzululumu pesa hizi indirectly,just imagine kwa wale wanaofanya kazi taasisi binafsi......Mfano mkataba umeisha baada ya miaka mi 3 na kampuni haina uwezo wa kuendelea nae,sasa kama ana ki milion 6 chake na ana umri wa miaka 28,je akifikisha umri wa miaka 60 hiyo million 6 ataweza kuifanyia nn?atakapokuwa amefikisha miaka 60, million 6 itakuwa ni ela ya bia 5 na kuku choma 1.....kwa kifupi hiyo ela hutoweza kufanyia kitu ambacho ungeweza kufanyia leo.........Hiyo ela ingeweza kuwa mtaji wa kufanyia mambo mengine kwa sasa kama umepoteza ajira,waiache hii pesa.....................Serikali imekuwa ni choyo,binafsi na inatafuna ela zetu wanyonge.
 
Ndo nimeamini siasa za kiAfrika ni siasa uchwara,yaani hapo ni kama wameamua kuzululumu pesa hizi indirectly,just imagine kwa wale wanaofanya kazi taasisi binafsi......Mfano mkataba umeisha baada ya miaka mi 3 na kampuni haina uwezo wa kuendelea nae,sasa kama ana ki milion 6 chake na ana umri wa miaka 28,je akifikisha umri wa miaka 60 hiyo million 6 ataweza kuifanyia nn?atakapokuwa amefikisha miaka 60, million 6 itakuwa ni ela ya bia 5 na kuku choma 1.....kwa kifupi hiyo ela hutoweza kufanyia kitu ambacho ungeweza kufanyia leo.........Hiyo ela ingeweza kuwa mtaji wa kufanyia mambo mengine kwa sasa kama umepoteza ajira,waiache hii pesa.....................Serikali imekuwa ni choyo,binafsi na inatafuna ela zetu wanyonge.
hahahaha aiseeeeeeeh
 
Vp kwa wale ambao tayari hawapo kazini zaidi ya mwaka na zaidi kabla ya sheria hii haijapita,je na wao utaratibu huu unawagusa? Navyoelewa sheria hua hairudi nyum
 
Kuna watu wanakismart ya umaskini katika utawala, hata wajitahidi vip maisha Ya wananchi yanazidi kuwa magumu
 
Back
Top Bottom