Mangi merry
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 221
- 41
SERIKALI inatarajia kuajiri
watumishi wa afya 5,000 nchini,
ambao wataanza kazi Mei Mosi mwaka
huu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Celina Kombani, alisema jana kwamba
wiki hii vibali vya ajira za
watumishi hao wapya vitatoka.
Mwakani tutaajiri watumishi
wengine wa afya 11,000 na
sehemu kubwa ya watumishi
hao wapya wa mwaka huu na
mwakani itakwenda vijijini,
alisema Kombani.
Alitoa maelezo hayo wakati
akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Chunya, Victor
Mwambalaswa (CCM), aliyetaka
kufahamu ni lini zahanati zilizokamilika kwa muda mrefu, zitapewa watumishi wa afya.
Wakati huo huo katika swali la msingi,
Mbunge wa Mufindi
Kusini, Menrad Kigola (CCM),
alihoji ni lini Serikali itamaliza
ujenzi wa vituo vya afya vya
Mtwango, Mninga, Mgololo na
Bumilayinga katika jimbo lake.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey
Mwanri, alisema Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi imeomba idhini ya Sh
milioni 420.5 kupitia Mpango wa
Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM),
ili kuendeleza ujenzi wa vituo vya afya,
zahanati na nyumba za watumishi.
Hata hivyo leo (jana) nimezungumza
na Mkurugenzi wa Halmashauri na hivi
vituo alivyotaja mbunge havipo, sasa
katika halmashauri yenu
angalieni upya vipaumbele
vyenu, alisema Mwanri.
Ujenzi wa vituo vya afya vya
Mtwango, Mninga, Mgololo na
Bumilayinga, ni miongoni mwa
miradi ya afya 21 iliyoibuliwa na
wananchi wa Mufindi Kusini, zikiwamo zahanati 17 na vituo vya afya vinne. Sehemu kubwa ya ujenzi umechangiwa na wananchi.
SOURCE; HABARI LEO
watumishi wa afya 5,000 nchini,
ambao wataanza kazi Mei Mosi mwaka
huu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Celina Kombani, alisema jana kwamba
wiki hii vibali vya ajira za
watumishi hao wapya vitatoka.
Mwakani tutaajiri watumishi
wengine wa afya 11,000 na
sehemu kubwa ya watumishi
hao wapya wa mwaka huu na
mwakani itakwenda vijijini,
alisema Kombani.
Alitoa maelezo hayo wakati
akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Chunya, Victor
Mwambalaswa (CCM), aliyetaka
kufahamu ni lini zahanati zilizokamilika kwa muda mrefu, zitapewa watumishi wa afya.
Wakati huo huo katika swali la msingi,
Mbunge wa Mufindi
Kusini, Menrad Kigola (CCM),
alihoji ni lini Serikali itamaliza
ujenzi wa vituo vya afya vya
Mtwango, Mninga, Mgololo na
Bumilayinga katika jimbo lake.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey
Mwanri, alisema Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi imeomba idhini ya Sh
milioni 420.5 kupitia Mpango wa
Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM),
ili kuendeleza ujenzi wa vituo vya afya,
zahanati na nyumba za watumishi.
Hata hivyo leo (jana) nimezungumza
na Mkurugenzi wa Halmashauri na hivi
vituo alivyotaja mbunge havipo, sasa
katika halmashauri yenu
angalieni upya vipaumbele
vyenu, alisema Mwanri.
Ujenzi wa vituo vya afya vya
Mtwango, Mninga, Mgololo na
Bumilayinga, ni miongoni mwa
miradi ya afya 21 iliyoibuliwa na
wananchi wa Mufindi Kusini, zikiwamo zahanati 17 na vituo vya afya vinne. Sehemu kubwa ya ujenzi umechangiwa na wananchi.
SOURCE; HABARI LEO