kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2016/17 zitazotumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la X-Ray katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
Hayo yalisemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua lini jengo la Maabara ya Mionzi linalojengwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya litakamilika.
Ummy alisema katika mwaka wa Fedha 2015/16 Tsh. Bilioni 8 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi huo, ingawa ujenzi huo haukufanyika lakini nia ya Serikali ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo uko pale pale.
Akiainisha matumizi ya pesa zilizotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17, Ummy alisema Tsh. Bilioni 3 zitatumika kuendeleza ujenzi pamoja na kulipa deni lililobaki kwa mkandarasi aliyekuwa anajenga na bilioni 2 zitatumika kununua vifaa tiba vikiwemo CT- Scanner na MRI.
Akijibu swali la nyongeza toka kwa Mhe. Catherine Magige (Viti Maalum CCM), Mkoa wa Arusha, Ummy alisema bilioni 9 zimetengwa kwa ajili mya kununua vifaa tiba ikiwemo kuweka CT-Scanner na MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa Wizara imepata kibali cha kuajiri wafanyakazi 10,000 wa afya nchini kati ya maombi ya kuajiri wafanyakazi 30,000.
Aliongeza kuwa Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha Hospitali za rufaa nchini ikiwemo ya Singida, Sekou Toure ya Mwanza, Mbeya na Arusha.
Ummy alisisitiza kuwa ni nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha sekta ya afya nchini na kuwafanya wananchi kuwa na afya bora.
Chanzo: Habari leo