Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 277 kila mwaka kwa ajili ya kugharamia huduma mbalimbali za Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI nchini, ikiwa ni hatua ya kupunguza utegemezi kwa wafadhili wa kimataifa katika mapambano dhidi ya janga hilo
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, Agosti 6, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Samwel Sumba, alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 32 ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, alipotembelea mabanda ya Ofisi ya Waziri Mkuu likiwemo banda la TACAIDS
Dkt. Sumba amesema kuwa uwekezaji huo mkubwa wa Serikali unaonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha afua za VVU na UKIMWI kwa kutumia rasilimali za ndani, hatua inayolenga kupunguza maambukizi mapya na kuboresha maisha ya watu wanaoishi na virusi hivyo
“Ni muhimu kwa nchi kuanza kujitegemea kifedha katika mapambano haya. Hii itasaidia kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwa uhakika hata kama misaada kutoka kwa wafadhili itapungua au kusimama,” amesema Dkt. Sumba
Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Athari za UKIMWI ya mwaka 2022/2023, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu wanaoishi na VVU kati ya 1,540,000 (milioni moja laki tano na arobaini elfu) hadi 1,700,000 (milioni moja laki saba). Kiwango cha maambukizi kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi ni asilimia 4.4, ambapo wanawake wanaongoza kwa asilimia 5.6, ikilinganishwa na wanaume wenye asilimia 3.0
Chanzo: Jambo TV