Serikali yatelekeza mgodi wa Kiwira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatelekeza mgodi wa Kiwira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kmp, Jun 10, 2010.

 1. kmp

  kmp Member

  #1
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yatelekeza mgodi wa Kiwira
  Katika taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) ya jana usiku imeonesha kwamba Serikali imeutelekeza mgodi mkuu wa makaa ya mawe wa Kiwira uliopo mkoani Mbeya, baada ya mgodi huo kutofanya kazi kwa miaka miwili mfululizo.


  [​IMG]
  Akielezea masikitiko yake kuhusu mgodi huo, meneja mkuu wa mgodi huo Abdul Haji amesema mashine za mgodi huo wa Kiwira tayari zimeanza kuchakaa, kutokana na shughuli yoyote kutoendelea hapo, huku buibui nao wakijenga maskani ndani yake.
  Amebainisha kuwa mgodi huo ulikuwa ukiipatia Serikali faida kubwa ya shilingi milioni 200 kila mwezi, kutokana na kuweza kuzalisha zaidi ya tani 8,000 za makaa yam awe, licha ya kuwapa ajira wakazi wengi wa maeneo ya karibu na mbali.


  Nao walliokuwa wafanyakazi katika mgodi huo, wamelalamika kuishi katika mazingira magumu, kutokana na kuachishwa kazi na kwamba wanaitaka Serikali kutazama upya uamuzi wake wa kuufunga mgodi huo, hasa kwa maslahi ya mashine zinazoendelea kuchakaa, mashine ambazo wamesema ni kodi za wananchi.  Kwa upekuzi niliofanya inaonesha kwamba mgodi wa kiwira unaweza kuzalisha mpaka megawati 200 za umeme na thamani ya mgodi mpaka mwaka 1991 ilikuwa ni bil 7.
  Sasa maswali ni:


  1. kwa tatizo la umeme tulilonalo hapa nchini, mgodi huu si ni rasilimali tosha ambayo ingepunguza matatizo hayo ya umeme?


  2. Hasara hii italipwa na nani kwani fedha zilizotumika kujenga mgodi ni kodi za wananchi


  3. Waziri wa Nishati na madini Bw. W. Ngeleja alitoa tamko bungeni kwamba


  4.Utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilolitoa kwa Wizara ya Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya mjadala wa bajeti yake, Juni 27 ,2008 na Juni 26, 2009 na ahadi ya Wizara ya Nishati aliyotoa waziri wake wakati wa majumuisho ya makadirio ya matumizi ya wizara yake Julai 9 mwaka jana kuhusu kujenga uwezo wa mashirika ya Shirika la Madini la Taifa (Stamico) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ili yamiliki na kusimamia mradi yamefikia wapi?


  5. Mazungumzo na Serikali ya China iliyoanzisha na kuendesha mradi huo, ili kupata mkopo wa kufufua mradi huo na kuhakikisha uzalishaji wa umeme wa megawati 200 unakamilika mapema umefikia wapi?  Sources:
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=2823


  Dar411.com: Dar-es-Salaam News and Information Portal:Serikali yalaumiwa kutelekeza mgodi wa Kiwira
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Bado tyuko busy na mpira wa brazil na world cup. Mambo ya nishati tutayazungumza baadae mwaka huu
   
Loading...