Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar

wanatoa bei elekezi kwenye unga tu, huo unga tutakula bila mboga.?
 
walitakiwa waje na mpango endelevu. hizo tani walizotoa ni za kuliwa na kuisha siku mbili. baada ya hapo nini kitafuata?? bei si itarudi palepale?? wakajipange upya aisee

Wafanyabiashara watanunua nafaka kwenye maghala kwa bei poa, wasafirishe nje au wasubiri kuja kuuza kwa bei ya juu. point yako inahusika sana, long term solution inahitajika.
 
Kwanini Dar, vp sehemu zingine za nchi, Mwanza sembe 1400/=, kuna wilaya zina njaa, chakula hamna, shilingi haionekani!
 
Kwanini Dar, vp sehemu zingine za nchi, Mwanza sembe 1400/=, kuna wilaya zina njaa, chakula hamna, shilingi haionekani!
 
Slogan ya "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" ilikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha malengo ya kwnda kukalia kiti. Kuna taarifa kupitia vyombo vya habari zilielezea kuwa utafiti unaonyesha asilimia 42 ya watoto hapa nchini wamedumaa hawakui. Kutokua vizuri ni kukosa lishe bora. Lishe bora ni sehemu ya "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" Kupanda kwa bei ya vyakula hapa nchini ni UZEMBE wa makusudi wa watendaji wa serikali wakati ndiyo hao hao wanaofanya utafiti. Bila shaka utafiti wanaoufanya ni kwa ajili ya kupanda ngazi zao za elimu kutoka digrii ya pili kwenda PhD, lakini tujiulize kwanini UNAUA WATU KWA MAKUSUDI KWA AJILI YA VYEO? Si busara kupanga bei ya SEMBE Peke yake, pangeni bei ya chakula kwa ujumla wananchi wanakufa. Kukosa milo kwa siku kunaongeza UHALIFU, FAMILIA KUHITILAFIANA, KWA UJUMLA NI TISHIO KWA USALAMA WA FAMILIA NA NCHI. Kupatikana kwa chakula cha kutosha huongeza watu kuzaana, utulivu, amani na maelewano. KWA MANTIKI HII SERIKALI INAHUSIKA KWA MAMBO MENGI SANA YA MAISHA YA WATU.

"MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA HAYAPO"
 
Siasa ni kitu cha ajabu sana,unasema ili tu watu wakusikie kama na wewe unaweza kusema...............kwa hiyo unga wote unaouzwa madukani utatokana na hayo mahindi kiduchu.tumesema soko huria,wacha lie huria.............supply mahindi kwenye soko,yenyewe yatashuka kwa dhana ya `demand and supply`na si vinginevyo.
 
Serikali yetu haiishiwi vituko. Kila siku wanahubiri juu ya athari za nafaka zilizokobolewa, leo hii wao ndio wa kwanza kukoboa mahindi na kusambaza madukani, hivi huwa tunapenda kuzungumza mambo tusiyo na muda wa kuyatekeleza?

Haya, kama hiyo haitoshi, unagawa mahindi kwa wafanyabiashara ambao huwezi kuwafuatilia na kujitapa kuwa bei itashuka. Hivi sio serikali hii hii iliyosema mtu akiuza sukari zaidi ya 1600 atakiona cha mtema- fire woods, lkn hakuna hata mangi mmoja aliyeshusha bei na mpaka leo tunanunua sukari 2000 - 2200 kwa kilo?!!
 
Hilo lengo haliwezi kutimia kwa sababu kwanza huo si mpango endelevu. Je hizo tani za mahindi zitatosha kulisha wana Dar hadi msimu wa mavuno utakapofika? Mimi nasema haiwezekani kama haiwezekani je mpango huo lengo lake ni nini? Ni kuwalambisha pipi Watz halafu baadaye waendelee na shida zao? Yaani hii serikali ni ya ajabu kweli! Mara zote mipango yao ni ya kukurupuka tu na wala si sustainable! Pia kwa kuwa hawana strict control mechanism mpango huu hautafanikiwa kamwe. Yetu macho. Serikali ya kifisadi haijawahi kufanikisha jambo la maana!
 

Wataalamu wanasema unga wa sembe haufai kwa afya ya binadamu kwa kuwa unakuwa umeondolewa virutubisho vyote, nina imani na serikali inalijua hili. Sasa iweje serikali ishauri matumizi ya sembe?

Bei na punguzwa DSM. Sisi wa mikoani je ?
 
Hawa jamaa kwa fix(changa la macho). Walishaiua tume ya bei na wakaliacha soko holele ! Atakaye uza unga kwa zaidi ya bei wanayoisema watamfanya nini na kama kutumia sheria, je ipo hiyo sheria katika nyakati hizi za soko huria. Sikujua kama kilo ya unga imefikia 1500/= dar. Huo ndio utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi. Cha kushangaza watanzania wanadhani hayo ndiyo maisha waliyopangiwa na Mungu. Tena ccm inaendelea kukaribisha wawekezaji kuja kuchukua ardhi zaidi. Wala hawaoni mbali na kujali. Wanadhani ardhi inaongezeka kama wanavyoongezeka watu. Kupigika kopte huku bado watu wachache wanakimbilia ccm. Kisa kuponya njaa ya siku 3!
 
Ule uchumi wa soko umeshindwa; si waliache soko liamue bei?

unajuna ni kwanini tunakwenda mbele hatua 5 na kurudi nyuma hatua 6? wanasiasa wetu hawajui siasa.essentially tupo katika mfumo wa kibepari na soko ndilo linatakiwa kuamua bei ya bidhaa lakini wanasiasa waongo wanalazimisha kupendwa.
 
nafikiri hiyo ni bei ya unga wao na hawana maana wanataka kuweka bei kwa soko lote la unga,siwapendi magamba lakini kwa hili nafikiri tusiwachukie bure
 
Unga tayari,mboga je? Tunataka nyama ishuke hadi 1000 kwa kilo
 
Serikali inalima wapi mahindi?
 
Hivi Tan 3000 inaweza kumaliza matatizo ya gharama za unga Dar ambayo inasemakana ina watu zaidi ya million 7??
 
hahaha..mfa maji haachi kutapatapa,bei ya unga iko juu Dar peke ake?
 
Bei mpya ya unga? serikali ya CCM sasa inauza UNGA? JK alienda Ufaransa kuangalia soko la UNGA? UNGA?
 
Mkipanga bei mkumbukeni pia mkulima ambaye ni masikini kule kijiji.....wanalima kwa taabu kubwa msaada wa serikali ni mdogo sana...serikali iongeze ruzuku katika kilimo ili angalau apate ahueni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…