Serikali yataifisha kilo 24 za dhahabu

Serikali yataifisha kilo 24 za dhahabu

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
47951ee9a6306e6c7871bc2128321ac9.jpg

SERIKALI imetaisha kilo 24 za dhahabu na 150 za vito vya thamani baada ya wamiliki wake kupatikana na hatia ya uhujumu uchumi. Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga amesema mjini Dodoma, pia kuna magari, nyumba na maghorofa ambayo walitaisha mwaka jana.

Amesema hayo baaada ya kufunguliwa mkutano wa waendesha mashitaka wa serikali nchini. Bila kueleza wamiliki wala ziliko nyumba hizo, Mganga alisema wamezuia maghorofa ya watu ambao wanaendelea na kesi za dawa za kulevya. “Tutaendelea kuhakikisha hakuna anayenufaika na uhalifu huu …tutahakikisha kuwa tunakurudisha ulikotoka,” amesema.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi, akifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi alisema lengo ni kuwajengea uwezo waendesha mashitaka kuhusu masuala yahusuyo dawa za kulevya. “Mwanasheria ili aweze kufanya kazi yake vizuri lazima ajue dawa za kulevya zinasambazwaje, madhara yake na mbinu zinazotumika na wauzaji, “ amesema Kilangi.

Alisema Taasisi ya Uchunguzi ya Taifa (NPS) haitaacha jiwe hadi ihakikishe wanaohusika na biashara hiyo wote wanachukuliwa hatua kali. Aliwahakikishia mali na bidhaa za wahusika wa uhujumu uchumi na dawa za kulevya zitataishwa na kuchukuliwa bila kujali cheo. Aliwaonya mawakili NPS kuwa wakishirikiana na wahalifu na ikabainika, hawatavumiliwa. Awali Waziri Kabudi alipongeza Jumuiya ya Ulaya (EU) iliyotoa fedha za kuendesha mafunzo yaliyowezesha serikali kupambana na dawa za kulevya na mipango ya uhujumu.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Kilangi alisema wachunguzi wanatakiwa kutumia fursa zao vizuri kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
 
Back
Top Bottom