kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
SERIKALI ilitangaza hivi karibuni kuboresha huduma za afya, zikiwemo za hospitali za rufaa, maalumu, kanda na hasa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kuiwezesha kutoa huduma ya kupandikiza figo.
Habari hii ni njema na itaiwezesha Serikali kuepuka gharama kubwa za kuwapeleka baadhi ya viongozi na maofisa wake nje ya nchi. Habari hii njema kwa Watanzania ilitolewa bungeni Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy alibainisha pia maboresho yatakayofanywa kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuwa ni kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU) kutoka 21 hadi vitanda 75. Pia akasema Serikali imeazimia kununua vifaa tiba vya upasuaji na kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 vya sasa hadi 18.
Aliongeza kwamba serikali itapanua huduma za kusafisha figo kwa kuongeza vitanda kutoka 15 hadi 50 na kuanza kusafisha figo kwa wagonjwa wenye Virusi Vya Ukimwi na virusi vya ini. Tunasema hii ni habari njema kwa Watanzania kwa sababu huduma za afya zimekuwa hazikidhi mahitaji ya Watanzania.
Mbali na kuwepo uhaba mkubwa wa dawa hospitalini hasa zile za rufaa, pia vifaa tiba, vyumba vya wagonjwa na madaktari vimekuwa ni kikwazo kwa wananchi kwa muda mrefu.
Wapo Watanzania wengi wamepoteza maisha kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kupata msaada, kwa kuwa ama hapakuwa na huduma za kutosha kwa maana ya kuwepo na wagonjwa wengi au kutokuwepo kwa huduma hiyo hapa nchini na ndio maana wenye uwezo wa kifedha tu, ndio walipelekwa nje ya nchi, hasa India, Uingereza na Afrika Kusini.
Kwa mfano, magonjwa yanayohusiana na figo, yamekuwa ni hatarishi kwa wananchi wengi kwa kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakihitaji gharama kubwa ya matibabu. Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli imeona hali hii na kuamua kuivalia njuga.
Kweli kuna kila haja ya kuendelea kuwaombea viongozi wa awamu hii, waweze kulitumikia taifa kwa mwendo huo huo wa kasi bila kikomo. Katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao, Muhimbili itaanzisha huduma mpya ya upandikizaji figo na upandikizaji kwa wagonjwa viziwi, itajenga jengo la kisasa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa binafsi na viongozi wa kitaifa na watu mashuhuri, litakalokuwa na vitanda 170 na kuongeza mapato kutoka Sh bilioni 2.6 za sasa hadi Sh bilioni 5 kwa mwezi.
Pia Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) katika mwaka wa fedha 2016/17, itaongeza nafasi ya wagonjwa wanaolazwa kutoka vitanda 150 hadi 340 ambapo katika chumba cha wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU) vitaongezeka kutoka vinane hadi 32.
Serikali imeazimia kununua mashine mpya za uchunguzi za MRI, CT Scan na X ray za dijitali na MOI itatoa mafunzo ya upasuaji wa marejeo kwa nyonga na goti. Tunaipongeza serikali kwa maboresho hayo makubwa ya huduma za afya na hatua mbalimbali za kuondoa kero za Watanzania.