Serikali yasema haina mpango wa kupanua Magereza nchini

Serikali yasema haina mpango wa kupanua Magereza nchini

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Serikali imesema haina mpango wa kutoa fedha kwa ajili ya kupanua Magereza yaliyopo na badala yake italitumia jeshi la polisi kupunguza uhalifu na kutoa adhabu mbadala kwa watu wanaokutwa na makosa mahakamani kama njia mbadala ya kukabiliana na msongamano wa wafungwa Magerezani.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mhe.Kangi Lugola ametembelea gereza kuu la Luanda jijini Mbeya kwa lengo la kujionea maisha halisi ya wafungwa na kushuhudia mlundikano wa mahabusu na wafungwa ndani ya gereza hilo na ndipo akatoa kauli kuhusu msimamo wa serikali katika kukabiliana na changamoto ya msongamano wa wafungwa katika magereza yote nchini.

Akiwa jijini Mbeya, waziri Lugola pia ametembelea maeneo yenye miteremko mikali ambayo yamekuwa na matukio ya ajali za mara kwa mara

Chanzo: ITV
 
Safi sana, Serikali itumie vyombo vyake kupunguza uhalifu na hivyo kupunguza wafungwa
 
Back
Top Bottom