Serikali yapoteza dola bil 1.5 sekta ya madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yapoteza dola bil 1.5 sekta ya madini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jun 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,753
  Trophy Points: 280
  Serikali yapoteza dola bil 1.5 sekta ya madini

  na Prisca Nsemwa, Bagamoyo

  Tanzania Daima~Sauti ya watu

  PROFESA Ammon Mbelle wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Uchumi, amesema kutokana na usimamizi mbovu wa serikali katika sekta ya madini, taifa linapoteza dola bilioni 1.5 kiasi ambacho kingeweza kusaidia katika bajeti kuliko kusubiri misaada ya wafadhili.

  Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo, wakati wa hitimisho la mchakato wa tathimini ya utawala bora nchini (APRM), alisema kiasi hicho ni mara kumi ya tunachokipata sasa hivi.

  Mbelle alisema hasara hiyo inatokana na serikali kuwaachia wawekezaji shughuli za madini kuendesha wenyewe pasipo yenyewe kuwa na ubia kitu ambacho ni hatari katika maendeleo ya nchi.

  “Hakuna mwekezaji anayeweza kuionea nchi yetu huruma kama sisi wenyewe tutajiweka pembeni katika shughuli ambazo zina tija kwa taifa kama sekta ya madini, kitendo ambacho kinatusababishia kupoteza mabilioni ya shilingi,” alisema Mbelle.

  Aidha alisema serikali lazima ibadilike kwa kufanya mikataba na wawekezaji kutokana na kupanda kwa bei ya madini katika soko la dunia.

  “Sisi bado bei yetu ya dhahabu ipo chini kutokana na mikataba tuliyoingia na wawekezaji, lakini sasa hivi dhahabu ipo juu katika soko la dunia kwa hiyo ufuatiliaji unahitajika kuinusuru sekta hiyo muhimu,” alisema Mbelle.
  Hata hivyo, alisema kutokana na tathimini ambayo wameifanya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, wameishauri serikali kufuatilia takwimu katika migodi mara kwa mara pamoja na kushiriki kwa asilimia 49 katika sekta ya madini
   
 2. Marlenevdc

  Marlenevdc Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sad, sad, sad truth!!
   
Loading...