Serikali yapata hasara 93bn/- barabara ya Dodoma- Manyoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yapata hasara 93bn/- barabara ya Dodoma- Manyoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jun 16, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Serikali yapata hasara 93bn/- barabara ya Dodoma- Manyoni

  Na Mwandishi wetu

  16th June 2009

  Barabara ya Dodoma- Singida.


  Serikali imepata hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 93.4 kutokana na ujenzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni-Singida yenye urefu wa kilometa 244 kuchelewa kukamilika.

  Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje aliliambia Bunge jana kuwa kutokana na hasara hiyo, gharama za mradi huo sasa, zinatarajiwa kuongezeka kutoka kiasi hicho cha fedha kufikia Sh. bilioni 205.4.

  Chibulunje alisema hasara nyingine iliyopatikana kutokana na kuchelewa kwa mradi huo, ni wananchi kuchelewa kupata huduma bora ya barabara mapema kama ilivyokusudiwa.

  Kutokana na hali hiyo, alisema serikali iliamua kukatisha mkataba na mkandarasi aliyepewa zabuni hiyo kutokana na kuchelewesha ujenzi wa barabara hiyo.

  Naibu Waziri huyo, alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Nzega (CCM), Lucas Selelii aliyetaka kujua sababu zilifanya ujenzi wa barabara hiyo kuchelewa, hasara zilizopatikana na lini mradi huo utakamilika.

  Alisema kati ya fedha zilizokadiriwa upya kugharimu ujenzi huo, Sh. bilioni 144.613 zinatarajia kutumika kujenga barabara hiyo sehemu ya Dodoma-Manyoni na Sh. bilioni 60.669 Manyoni-Singida.

  Chibulunje alisema mkandarasi anayejenga sehemu ya Mhala-Manyoni yenye urefu wa kilometa 17 ni Estim Construction Company Limited, ambaye anatarajia kukamilisha sehemu hiyo ifikapo Novemba, mwaka huu na yule wa sehemu ya Manyoni-Isunna (kilometa 54); kampuni ya China Geo Corporation (CGC), atakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ifikapo Desemba, mwakani. Hata hivyo, alisema hadi sasa jumla ya kilometa 173 za kiwango cha lami katika barabara hiyo zimejengwa na kukamilika.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  je hakuna penalty kutoka kwa mjenzi kufidia hasara kwa serikali? je huyo mjenzi alichaguliwaje? na adhabu kwa wahusika ikoje?
   
 3. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Huyo mjenzi ndie hana jina mpaka auliziwe?
   
 4. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sending a boy to do a man's job!!! Typical kichwa cha mwendawazimu wallahi!!
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Genlemen( and Ladiesof course) , read between the lines.
  1 Barabara ya Dodoma-Manyoni-Singida ni miradi miwili tofauti kabisa
  2 Barabara ya Manyoni Singida Mkandarasi ni Wachina na walifukuzwa zaidi ya miaka
  iliyopita
  3 Barabara ya Dodoma Manyoni Mkandarasi Konoike, AMEACHIA NGAZI baada ya ubababishaji mkubwa toka kwa mwenye kazi(zilisalia km 16 tu kukamilisha mradi)
  4 Ni vema wananchi kuuliza kiini cha kutotekelezwa/kutokamilika mikataba hiyo ili undani ufahamike
  5 Ni rahisi kuwalaumu Makandarasi lakini kuna ufisadi mkubwa uliojificha toka kwa mwenye kazi
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa mchango wako, sasa ni juu wabunge kulikazania hili iweje uzumbe wa watu wetu wenyewe uingizie serikali yetu hasara, ambazo zinaweza kuepukika? Hususana wabunge wenye kuguswa na hii barabara na wale wenye kuguswa na upotevu wa pesa , maana imekuwa kama wimbo wataifa sasa .
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Bw. Mramba, Bw. Mgonja na Bw. Yona walishitakiwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh. bilioni 13.7 (ambayo ni 15% tu ya hii hasara). Wakikaa kimya kwa hili tutawashangaa.
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hivi kitu gani hawa viongozi wetu wanaweza kufanya? wakati ujenzi unacheleweshwa walikuwa wanafatilia? na kama walikuwa wanafatilia kwanini maamuzi hayakufanyika mapema zaidi?
   
 9. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  The Contractor is supposed to cover the client with insurance (performance Bond) when awarded these projects.
  If the contractor failed to deliver what happened to the insurance? Why is the Government footing the loses?

  Inaelekea kuna mambo ya ufisadi yamejificha ndani yake na serikali inataka kuyaficha bila kueleza wananchi ukweli.
  Ni desturi ya serikali (TANRoads) ku-award construction contracts kwa makandarasi walio-bid kwa bei ya chini na ambao hawana uwezo wa kukamilsha projects as long as wanapata 10% yao. Inapofikia mahali wameshindwa ku-deliver wanakuwa terminated na kutafuta mkandarasi mwingine. this trend have been thehe all the time and construction costs normally doubles.

  Kwa nini hawa wanaofanya uzembe huu hawaadhibiwi? (10% goes on the way to the higher level)
   
Loading...