chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,850
- 29,572
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewaomba radhi wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini, kwa kuchelewa kuwafikishia fedha zao za kujikimu. Hata hivyo, aLIsisitiza kuwa tangu juzi fedha hizo zilishatoka Hazina.
Akizungumza bungeni janaalipokuwa akitoa majibu ya mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM), Mwigulu aliagiza taasisi zinazohusika kuacha shughuli zote, ikiwemo vikao ili kuhakikisha fedha hizo zifike kwa wanafunzi hao jana.
"Serikali imeshatoa fedha, naagiza taasisi zipeleke fedha hizo leo hii hii ili wanafunzi wasome tupate wataalamu wazuri…hii haitatokea tena," alisema Nchemba.
Awali, Bulaya aliomba Mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Lediana Mng'ong'o na alipopewa nafasi, alisema wanafunzi 6,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamegoma kwa kuwa hawajapelekewa fedha hizo na hawana ugomvi na kitu kingine.
Kwa mujibu wa Bulaya, wanafunzi hao wanaipenda Serikali yao, lakini kuchelewa kwa fedha hizo, kumesababisha mateso kwa wanafunzi hao ambao wengi ni watoto wa masikini wanaotokea vijijini, huku wanafunzi wa kike wakiathirika zaidi.
Bulaya alisema hata jana alipokuwa akizungumza bungeni, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam, kilikuwa kimefikia uamuzi wa kurejesha nyumbani wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza, kutokana na uchelewaji wa fedha hizo na kutaka Serikali ieleze kwa nini imechelewesha fedha hizo.
Akifafanua sababu ya kuchelewa kwa fedha hizo baada ya kuomba radhi, Nchemba alisema Hazina iliamua kubadilisha utaratibu wa utoaji wa fedha kwenda maeneo mbalimbali.
Alisema kwa utaratibu huo mpya, iliamuliwa kuwa fedha zinazotakiwa kwenda katika mifumo rasmi, ziwe zinapewa kipaumbele kwa kupelekwa kwanza kabla ya maeneo mengine ili uchelewaji wa fedha hizo usitokee tena.
Wanafunzi hao waligoma kuingia madarasani kuendelea na masomo juzi na kufanya mkutano chuoni hapo, kushinikiza Serikali kuwalipa fedha zao za kujikimu.
Kwa mujibu wa mkataba kati yao na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, fedha zinatakiwa kulipwa wiki ya 8 baada ya kusainiwa kwa mkataba baina yao na Serikali, lakini mpaka juzi ilikuwa wiki ya 11 bila malipo hayo.
Wanafunzi hao walisema hawana nia ya kufanya fujo za aina yoyote, bali wanachohitaji ni kupata suluhu ya tatizo hilo, ambalo limewaathiri kimasomo na kisaikolojia.
Waziri wa Mikopo wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Shitindi Venance, alinukuliwa akisema kuwa matatizo hayo yanatokana na mfumo mbaya wa mamlaka yenye dhamana ya kukusanya fedha za mikopo kwa walioajiriwa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alikiri madai ya wanafunzi hao 7,000 kati ya zaidi ya 10,000 wanaofadhiliwa na Serikali.
Lakini, alisema tayari amezungumza na Bodi ya Mikopo ambayo imemwahidi kuleta fedha hizo haraka, na kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.
UDSM warejea darasani Lucy Ngowi anaripoti kuwa mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Sehemu ya Mlimani ulioanza Jumatatu wiki hii, umemalizika baada ya juzi jioni wanafunzi zaidi ya 6,000 kulipwa fedha zao za kujikimu walizokuwa wanazidai.
Licha ya Serikali kulipa Sh bilioni 2.8 na kumaliza mgomo huo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema wanafanya tathmini kuona kiwango cha uharibifu kilichotokea katika hosteli ya Mabibo, pamoja na kuwabaini wote walioshiriki ili kuwachukulia hatua stahiki za kinidhamu.
Mukandala alisema hali chuoni hapo ni shwari baada ya wanafunzi hao kuingiziwa fedha zao juzi, hivyo wanafunzi wameingia darasani kuendelea na masomo yao.
Aidha, alisema wanafunzi wawili waliopata majeraha katika vurugu zilizotokea katika hosteli ya Mabibo, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri.
Chanzo: Habari Leo
My Take : Bado Madaktari, Waalimu na kada nyingine wanatakiwa kupewa haki zao, au mpaka na wao wagome kama walivyofanya Wanavyuo na kupewa haki zao?
Nina imani huu ndiyo wakati muafaka kwa kikundi chochote kudai haki na kutimiziwa maana tunaelekea Uchaguzi mkuu, serikali yetu itakuwa sikivu kwa kipindi hiki.