Serikali yangu imefumba macho??

Serikali yangu imefumba macho??

Muuru

Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
29
Reaction score
5
Wakuu nawasalim popote mlipo.
Kiukweli nashangazwa sana napopita maeneo ya Dar haswa Temeke na mnazi mmoja kuna watu wanaoendesha maonesho ya kuhusu freemanson na matumizi ya kondom
Kwa yeyote aliyewahi kuwaona watu hawa wanawadanganya watu eti wao walikua fremanson wakakimbia(sina uhakika kama mtu anaweza kuwakimbia wale majamaa)
Kikubwa ni hawa wanaodemo na kupinga matumizi ya kondom wakisema ina madhara makubwa kwa afya. Kiukweli ni umati mkubwa sana huenda kushuhudia. Swali langu ni Je,serikali imewapa vibali watu hawa? Kama ndio inafuatilia kujua matumizi ya vibali hivyo?
Pili ni Je,kwa umati wote ule hata kama sio wote wataafiki ila wakitoka watu watano walioaminishwa kwamba matumizi ya kondom ni hatari kwa afya na wakauza mechi kwa watu walioko kwenye mtandao madhara yake yatakua kiasi gani kwa jamii?
Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom