Serikali yalamba matapishi yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yalamba matapishi yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, Dec 17, 2009.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi bakuli la serikali analolitembeza rais wetu mheshimiwa sana JMK kwa watu weupe na lile bakuli la ombaomba Matonya je zina utofauti?
  Matonya alikuwa mzee, wengine hawana mikono, miguu, elimu na WENGINE wagonjwa.Lakini kwa amri ya makamba aliwafukuza KWAMBA hawastahili kuomba.kati ya wawili hawa ni nani anastahili kuwa omba omba?Kati ya hayo matatizo(uzee, ugonjwa, ukosefu wa viungo,matatizo ya akili, ukosefu wa mitaji nk) Je serikali yetu ina matatizo yepi? Matonya (na wengine)aliomba kwa chini ya miaka 30 nasikia kajenga nyumba, kaoa mke na ana watoto wanaenda shule je serikali yetu baada ya kuomba kwa miaka 48 wamefanya nini? (Unganisha na ile picha ya shule ya msingi huko kigoma wanafunzi wanasoma nje,wanawake wakijifungua chini kwenye HOSPITALI tena YA WILAYA, zile za bara bara za shinyanga wakati wa Mvua, Migomo ya wafanyakazi wa umma kwa sababu ya mishahara duni na matat, matatizo ya umeme njaa za kila mwaka etc).Na kama tumeomba miaka 48 na hadi leo hatujitoshelezi kwa basic needs, matatizo na madeni ya nje ndo yameongezeka kwa nini hatufikirii kama sisi na kutenda kama sisi badala ya kutenda kama mabwana zetu wanaovyotuelekeza?
  JE dhamira yetu ya kuchagua kingozi je si ili asimamie rasilimali yetu na atuongoze namna ya kuyatumia ili kufikia maendeleo na si aende kuomba msaada? NMB wanaanzia Tshs 50,000 KUWAKOPESHA WAJASIRIAMALI WANAAMINI NI KIANZIO TOSHA KWA BIASHARA YA MAANDAZI na wengine wamefanikiwa. Je benki kuu ya Tanzania kuna Shilingi ngapi? Huo mtaji ameshindwaje rais wetu kuuzalisha? KUNA WAFANYABIASHARA MMOJA MMOJA NCHINI MWETU WAMEFANIKIWA KWA NINI WASIINGIE UBIYA NA SERIKALI WAKAENDESHA UCHUMI wetu?Kama hamuwaamini je mbona tulikuamini? kama hakuna ubunifu kwa baraza lake la mawaziri si awanunue watalaam au consultants kwa gharama yoyote ile wamsaidie? HIVI UKIWA RAIS JUKUMU LAKO NI SIASA TU MBONA MKUU WETU HATEMBELEI VYOU VIKUU, VIWANDA ili ajue mahitaji ya technologia huko? ziara za ndani ni za kufungua majengo,na kuongea na viongozi wa chama basi?.TUBADILIKE
   
Loading...